Mambo ya kuzingatia katika ndoa

Mambo ya kuzingatia katika ndoa

Hellow it ia another Monday mtu wangu wa nguvu, kama kawaida yetu kwenye segmenti yetu ya mahusiano mapema tu leo tumekuja na mada Atari kabisa ambayo itakupa ufahamu mbali mbali.

Sasa watu wengi wanachukulia ndoa ni kitu au jambo la kawaida tu lakini kuna mambo kadha wa kadha ambayo unatakiwa kuyafamu, leo bwana nimekujia na vitu ambavyo unatakiwa kuvizingatia katika ndoa kwa wote mke na mume. Na hii si kwa wanandoa tu bali kwa wachumba ambao wanakaribia kufunga ndoa na mahusiano

Mambo yakuzingatia katika ndoa na uchumba au mahusiano

1.Wote jitahidini kucheka pamoja

Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mnaweza kucheka pamoja pia kulia pamoja, hii inafanya kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote.

 

 Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu  Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea  Kama utaanza kujizoeza  hivi ukiwa nyumbani, taratibu  utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.

2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo Onyesha heshima katika vitu hivyo pia  Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu.  Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye  Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo  Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua  na sisi pia.

3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote  Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu wa kimwili.  

Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani) Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.


4.Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano  Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao  Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu,  Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu.

Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu ikiwemo changamoto unazi kumbana nazo.

5.Samehe na kubali kusamehewa na kusahau yote

Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yenu Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia.

 Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yenu  Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu  Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.

6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko  Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano  wetu lazima ume halisi na sio feki  Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu.

Ukianza kupata  ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags