Mambo ya kuzingatia kabla ya kuchagua kozi ya kusoma chuoni

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuchagua kozi ya kusoma chuoni

Aaaaweeeeeeh! I hope mko poa kabisa wanangu wa vyuoni. Kama kawaida yangu siwezi kuwatupa hata siku moja kwenye ile segment yetu pendwa ya kujuzana mambo mbali mbali yanayohusiana na maswala ya vyuoni.

Kama tunavyojua hivi karibuni makontena mapya yataingia chuoni yaani wanafunzi wapya. Leo tutazungumza nao kuhusiana na mambo gani ya kuzingatia kabla ya kuchukua kozi ya kusoma, usichague tu kisa rafiki yako nae amechagua au usichague kisa mzazi kasema, tafakari kwanza ndo ufanye maamuzi.

Kuchagua kozi utakayoisoma chuo ni moja ya maamuzi makubwa sana unayoweza kuyafanya kwaajili ya maisha yako. Maana yanaathiri utakachosoma kwa miaka yako utakayokuwa chuo na utakachofanya baada ya chuo na pengine maisha yako yote.

Chukua muda kufikiria kwa kina, najua mpaka ulipofikia unajitambua haswa, usikubali wazo lolote unalopewa ilimradi uende chuo na upate boom umalize urudi kwenu.

Mambo ya kuzingatia kwenye kuchagua kozi

  1. Angalia passion yako

Siri kubwa ukianza kazi unaweza kufanya muda mrefu sana katika hilo eneo ambalo unakuwa umesomea kutokana na kozi hiyo.

  • Je, una passion na hayo mambo au unapenda kufanya hiyo kazi na je unaendana nayo, uwezo unao wa kukabili changamoto na mengineyo.
  • Vitu gani vinakufanya upate furaha ya kuishi?Na hivyo vitu vinaingiaje kwenye kazi utakayoipata kwenye hii kozi unayotaka kuisoma?
  • Ujuzi utakaoupata ndio utakaokusaidia kwenye kazi unayoitaka?
  1. Angalia kombi uliyosomea na kazi ya ndoto yako

Kombi uliyosomea inakupelekea kujua kozi gani unaweza soma chuoni. Lakini pia ni kazi gani ambayo toka zamani ulikuwa unatamani kuifanya? Na je kozi hiyo inakupelekea kuifanya hiyo kazi?

  1. Jiulize kwanini unataka kusoma kozi hiyo

Usisome kozi tu kisa umeambiwa inaajira nyingi, soma kozi unayoipenda na ambayo itakuwa na faida kwako. Mfano,

  • Upatikanaji wa ajira?
  • Gharama za kujisomesha kozi hiyo unazimudu?
  • Kozi hiyo unapata boom 100%

Natumai sijachelewa sana kuwajuza swala hili huu ni muda wako wa kufanya maamuzi sahihi ili usije kujuta badae

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags