Mambo anayotamani kuyafanya kocha Eriksson kabla hajafa

Mambo anayotamani kuyafanya kocha Eriksson kabla hajafa

Baada ya kuweka wazi kuhusiana na kubakiza muda mchache wa kuishi ‘kocha’ wa zamani wa ‘timu’ ya Taifa ya England Sven-Goran Eriksson ameachia list ya mambo ambayo anataka kuyafanya kabla hajapoteza maisha.

Aidha kwa mujibu wa #Skynews Eriksson ameweka wazi kuwa kwa siku hizo zilizosalia anampango wa kusafiri nchi mbalimbali na kuhudhuria ‘mechi’ nyingi, huku akitamani kushuhudia ‘mechi’ ya England dhidi ya Brazil inayotarajiwa kuchezwa mwezi Machi, 23 mwaka huu.

Sven-Goran Eriksson alifunguka kuhusu afya yake siku mbili zilizopita kuwa anasumbuliwa na saratani ya kongosho ikiwa hatua ya mwisho huku akieleza kuwa amebakiza mwaka mmoja wa kuishi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags