Mambo 6 ya kufanya ili kuwa bora zaidi

Mambo 6 ya kufanya ili kuwa bora zaidi

Ni siku nyingine tena Jumatatu tulivu kabisa tunakutana kujuzana mambo mbalimbali ambayo najua wewe mwanafunzi yanaweza kukusaidia hao ulipo chuoni.

Basi leo karibu nikufahamishe mambo 10 ambayo unaweza kuyafanya kuanzia sasa ili uweze kuwa bora zaidi.

  1. Jifunze lugha mpya

Moja ya jambo unalopaswa kujifunza ili uwe bora zaidi ni kujua lugha mpya, kama unajua Kiswahili peke yake basi una budi kujifunza na lugha ya kingereza.

Kufanya hivyo kutakuongezea wigo wako wa maarifa na fursa mbalimbali zinazoweza kujitokeza mbele yako.

  1. Shinda hofu na wasiwasi

Najua hofu na wasiwasi ni mambo ambayo yamekuwa yakiwakumba wanafunzi wengi na hali hiyo uwafanya kuhsindwa kufikia malengo yao kwa wakati.

Sasa ili iweze kuwa bora zaidi unapaswa kushinda hofu na wasiwasi, nasisitiza ili uweze kufanikiwa shauku yako lazima iwe kubwa kuliko hofu ya kushindwa.

Sisi sote tuna hofi mbalimbali, hofu hizi hutuzuia tusifanikiwe au kukua, ni wazi kuwa ili kuwa bora zaidi, ni lazima tushinde hofu na mashaka ambayo mara nyingi hutawala maisha yetu na kutupotezea mafanikio yetu.

Tukishinda hofu tutathubutu kufanya mambo mbalimbali kwa ajili ya kufikia malengo yetu.

  1. Boresha ujuzi wako

Najua wanafunzi wengi huko vyuoni tumejaaliwa kuwa na ujuzi fulani, basi ukiwa na ujuzi fulani hakikisha unauukuza na kuuendeleza uwe bora kabisa.

Ikiwa wewe ni mjasiriamali, mbunifu, fundi au msanii hakikisha unajenga uwezo na maarifa yako yawe bora kabisa, kila mara hakikisha unajifunza mambo mapya yanayohusiana na ujuzi wako.

  1. Amka mapema

Haaaa hapa nacheka kidogo na hiyo ni kwa sababu najua wanafunzi mliowengi ni wavivu sana wa kuamka mapema asubuhi.

Sasa unaambiwa kuamka mapema ni jambo ambalo linaweza kukufanya kuwa bora zaidi ikiwa utalifanya kwa uhakika.

Kuamka mapema kutakupa fursa ya kutumia muda vyema hasa wa asubuhi ambao mwili na akili vinakuwa viko vizuri kiafya.

  1. Fanya mazoezi

Kufanya mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kujenga afya zetu. Unaweza kukimbia, kupiga push up, kuruka Kamba, kunyanya vyuma na mazoezi mengine madogo madogo.

Kwa njia ya mazoezi unaweza kuimarisha na kulinda afya ya mwili wako, jambo hili litakufanya kuwa bora zaidi na kuwa na ufanisi mkubwa katika masomo yako.

  1. Jiwekee malengo

Unajua baadhi ya watu hawana kabisa utamaduni wa kujiwekea malengo, basi leo tunakujuza kuwa ili uweze kuwa bora zaidi huna budi kujiwekea malengo.

Malengo yatakuwezesha kufahamu unataka kufanya nini, lini, wapi na kwa namna gani.

Tambua kuwa ni muhimu sana kujiwekea malengo katika maisha yako na kila siku hakikisha unafanya kitu ili kuelekea malengo yako






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags