MAMA mzazi wa Hamisa Mobetto aitwae Shufaa Lutenga maarufu 'Mama Mobetto 'amefichua siri akieleza siku ya kwanza mkwewe, Stephane Aziz Ki kukutana na Hamisa Mobetto alimtamkia anataka kumuoa.
Mama Mobetto amesema, Hamisa alimwambia siku ya kwanza kukutana na Azizi Ki alimwambia anataka kumuoa na sio kuwa mpenzi tu.
"Mimi na Hamisa jinsi tunavyoishi huwa hatufichani kitu, na siku ya kwanza Hamisa kukutana na Azizi Ki alikuja kuniambia kuwa alimtamkia anataka kumuoa, sikuamini," amesema Mama Mobetto.
Mama huyo, amesema, Hamisa na Azizi Ki wapo katika uhusiano mwaka moja hadi kufikia hatua ya sasa ya kufunga ndoa ni jambo la kheri sana.
Amesema, anamshukuru Mungu Kwa tukio hili, kwani kuna mambo mengine mabaya yameongelewa kwake, ila Mungu ndio mtu wa mwisho mwenye kuamua kila kitu," amesema mama Mobetto na kuongeza;
"Yamepita mambo mengine sana mazuri, na mabaya mengine sana, ila nashukuru Mungu kwa kila kitu, Hamisa ni mtoto wangu wa pekee nilikuwa naumia sana na maneno ya watu huko mitandaoni na wengine nje ya mitandao. Sasa ni wakati wa furaka kwake mwanangu."
Mama Mobetto amefungukia pia, Aziz Ki ndiye aliyemvalisha siku ya leo ya kupokea mahari.
"Kiukweli nimepata mkwe mwenye upendo sana, hizi nguo za leo nilizovaa ameniletea yeye, gauni hili ni Sh 5 milioni, pochi milioni nne," amesema Mama Mobetto.
Imeandikwa na Rhobi Chacha

Leave a Reply