Mama Kim Kardashian afanyiwa upasuaji

Mama Kim Kardashian afanyiwa upasuaji

Baada ya mfanyabiashara na mama mzazi wa Kim Kardashian, Krish Jenner kudai kuwa anatatizo la kiafya, sasa mwanamama huyo ameweka wazi kuwa kutokana na tatizo hilo amefanyiwa upasuaji.

Krish Jenner ameyasema hayo kwenye reality show ya ‘The Kardashians’ akiwa na watoto wake Kim, Kendall, Khloe pamoja na mpenzi wake Corey Gamble kwa kuweka wazi kuwa alifanyiwa upasuaji na kutolewa uvimbe kwenye ovari yake.

“Nilitaka kuwaambia kitu kwa sababu nilikuwa sijawaambia bado. Nilikwenda kwa daktari, na kufanyiwa upasuaji, madaktari walikuta uvimbe mdogo kwenye ovari yangu ambao ilipelekea kutolewa kabisa” Krish Jenner alieleza huku akitokwa na machozi

Ukiachilia mbali kufichua ukweli kuhusu afya yake kwa familia yake pia ameeleza kuwa kuondolewa kwake ovari zote kumemuathiri kihisia ndio maana hayupo sawa kwa siku za hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa Krish Jenner alitoa taarifa ya kuwa na tatizo la kiafya mwanzoni mwa mwezi Mei wakati alipokuwa akizungumza na watoto wake kwenye reality show yao iliyoanza kuoneshwa Mei 23 mwaka huu.

Krish Jenner ni mama wa watoto wafanyabiashara na wanamitindo maarufu Kylie Jenner, Kim Kardashian, Kendall Jenner, Khloé Kardashian, Kourtney Kardashian, Rob Kardashian aliowapata na marehemu mumewe Robert Kardashian.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags