Mali za MJ zasababisha mgogoro kwa familia

Mali za MJ zasababisha mgogoro kwa familia

Familia ya marehemu mfalme wa Pop kutoka nchini Marekani Michael Jackson (MJ) imeripotiwa kuwa na mgogoro wa mali baada ya mtoto wa mwisho wa MJ, Bigi Jackson maarufu kama MJ Blanket (22) kukataa bibi yake Katherine (93) kutumia mali za baba yake (MJ) katika kesi inayoendelea mahakamani.

Kwa mujibu wa tmz wameripoti kuwa kulingana na hati zilizofika ofisini kwao zinaonesha kuwa MJ Blanket amewasilisha ombi katika mahakama nchini humo kutomruhusu bibi yake kutumia pesa za MJ kwa ajili ya kukata rufaa.

Ikumbukwe kuwa MJ Blanket na bibi yake mwanzo walikuwa wakishirikiana katika kesi ya kuwazuia wasimamizi wa mali za MJ kufungua biashara ambayo itaghalimu kiasi kikubwa cha pesa.

Aidha kwa mujibu wa ripoti hiyo Blanket aliweka wazi kuwa amefanya hivyo kutokana na kutoona kama kesi hiyo itashinda.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags