Makosa ya uvaaji unayopaswa kuyaepuka

Makosa ya uvaaji unayopaswa kuyaepuka

Mambo vipi watu wangu wa fashion? Halooo ni wiki nyingine tena tunakutana bwana kama ilivyo kawaida yetu hii ndiyo sehemu pekee ya kufundishana mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya fashion.

Wiki hii bwana nimekusogezea mada hii hapa makossa ya uvaaji unayopaswa kuyaepuka bwana.

Kama unavyofahamu kuna wale ambao wanavaa nguo kwa kuzingatia muonekano na muktadha husika, halafu bwana kuna wale wenzangu na mimi ilimradi tumevaa potelea pote hahaha hiyo haifai bwana acha leo tuelimishane hapa.

Makosa ni kitu cha kawaida hususani katika uvaaji, Hata kwa watu wanaojua kuvaa kuna siku unakosea step. Ni makosa ambayo kwa hatua chache kadhaa yanaweza kurekebishwa.

 Kurekebisha makosa haya kutasaidia kuboresha style yako na uvaaji wako na pia inaweza kusaidia hata kupunguza matumizi yako katika mavazi. Tumia maelezo haya kuboresha manunuzi, upangiliaji na uvaaji wako.

  • Kununua mavazi bila mpangilio

Ushawahi jikuta una harusi lakini kila siku unajivuta kununua nguo hadi inafika siku moja kabla ya harusi au asubuhi yake ndio uko busy unazurura insta kuangalia nguo unakosa unaenda dukani hapo hata nywele hazijakaa sawa mwisho wa siku unakuja kununua nguo ambayo huna uhakika unaipenda au lah? Ndio huku kukosa mpangilio. Ni vizuri kupangilia unachotaka na pia kujipa muda hususani unapoenda kununua mavazi. Angalia una nguo zipi na ni nguo aina gani ukiongeza si kwamva itakusaidia tu katika tukio la siku moja bali itakuwa nguo itakayokusaidia hata siku za mbeleni.

 

  • Kununua kitu kwa sababu tu ina punguzo la bei

Kuna wakati ukiona kitu kilichokuwa kinauzwa bei ghali kimeshuka sana bei unapata uchizi, si kwamba unakihitaji kweli ila basi tu kinavutia fulani na bei ni ndogo sana hivyo unaona ununur hata kama utaishia kutunza kabatini. Jiulize una nguo, mikoba au viatu vingapi uwa inapita hata miezi haujavaa! Kama una vitu vingi vya namna hiyo basi una hili tatizo. Kabla ya kununua kitu hata kama ni cha ofa jiulize mara mbili kama unakihitaji kweli, utakivaa wapi? Kama unaona si muhimu sana basi achana nacho.

  • Kutorekebisha nguo na viatu mapema

Unavaa kiatu mpaka kinatia huruma kabisa. Siku ukiamua kukikarabatu inakuwa too late. Sio viatu tu bali hata nguo. Kufanyia nguo na viatu marekebisho MAPEMA itasaidia udumu na vitu kwa muda mrefu hivyo kuondoa ulazima wa wewe kununua vitu vipya kila wakati.

  • Kukosa mpangilio wa vitu vyako

Naposema vitu namaanisha viatu,nguo,mikoba,nakshi. Yani kila kitu kipo kila kona. Kuna wakati tunachoka au mambo yanakuwa mengi lakini ni muhimu kutafuta hata siku moja katika wiki kwa ajili ya kupanga vitu vyako. Kwanza utajua una nini na hauna nini, itakuwa rahisi kwako kupangilia muonekano, vitu vitadumu muda mrefu kwasababu vunatunzwa vizuri . Unaporundika nguo inakuwa ngumu kwako kuvaa kila nguo hivyo unajikuta unarudia nguo zile zile zilizopo juu zaidi. Jitahidi kupangilia vitu na kuvitenganisha.

 

  • Kubeba mkoba ule ule kila sehemu na katika kila tukio

Kuna ule mkoba unaupenda sana, ndio unaotunza vitu unavyohitaji kila siku. Kuhamisha vitu kila saa ni mtihani lakini lazima kuna sehemu huo mkoba hautafaa. Mkoba wa kazini hautapendeza kwenye nguo nzuri ya party. Kuna nguo ni casual sana zinahitaji begi la mgongoni au mkoba fulani simple sana. Kitu kidogo kama mkoba kinaweza haribu vazi lako. Jitahidi kuwa na mikoba kadhaa kwa ajili ya matukio tofauti. Sio lazima iwe mingi ila uwe na mkoba au pochi kwa ajili ya mchana, usiku, n.k.

 

  • Kutomthamini fundi Juma

Unamuona yule fundi cherehani? Yule ana uwezo wa kubadilisha kabisa uvaaji wako, anaweza kukusaidia kupunguza matumizi ya pesa na anaweza kukusaidia uvae nguo ambazo haukutarajia utazivaa. Jenga tabia ya kupeleka nguo zako kwa fundi kwa ajili ya matengenezo. Kuna nguo pia huwa tunaforce kuvaa, mtu unajua fika hii nguo ina tatizo ila unajipa moyo hakuna tatakayeona. Jiondolee stress ya kujishtukia kila saa na kujikagua peleka hiyo nguo kwa fundi. Mara nyingi fundi wana bei ndogo. Kama nguo kubwa kapunguze, haina kitu kaweke, ina kitu cha ziada kapunguze. Kuna nguo nzuri za mtumba zinazouzwa kwa bei ndogo ila zinahitaji tu fundi so mtumie fundi Juma.

  • Kung’ang’ania vitu usivyovitumia tena.

Kwanini hutaki kugawa kitu ambacho haukitumii? Trust me ipo siku hautakuwa nacho tena. Gawa, wape wadogo zako, mtu mwembamba au mnene zaidi ambaye hiyo nguo itamtosha au watu wasiojiweza. Tupa hayo makopo matupu ya lotion,perfume na poda nunua urembo huo sio urembo.

  • Kupuuzia vitu vidogo vidogo

Umevaa blauzi haina mikono na bra yako ina rangi ya orange wakati top ni kijani, mikono ya vest yako imelegea, nguo inaonyesha sana, suruali inabana sana kiuno au inashuka kila saa. Haya ni matatizo madogo madogo tu ambayo mara bnyingi tunayapuuzia. Jitahidi kuyarekebisha yasije kukuaibisha.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post