Mahakama nchini Argentina imetoa hukumu kwa Cristina Fernandez de Kirchner (69), kutokana na makosa ya rushwa ambapo amedaiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kutoa kandarasi ya umma kwa rafiki yake.
Hata hivyo hataweza kutumikia kifungo hicho hadi rufaa yake itakapokamilika ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni kupinga hukumu hiyo.
Ataendelea na nafasi yake ya Umakamu wa Rais huku kesi ikipitia mahakama ya juu. Fernández amesema hukumu hiyo ni ya kisiasa na kuitupia lawama mahakama kwa kushiriki katika 'michezo michafu.’
Leave a Reply