Maji ya mchele yanavyo weza kukuza nywele zako

Maji ya mchele yanavyo weza kukuza nywele zako

Na Asha Charles

Hellow niaje watu wangu wa nguvu!!! I hope mko salamaa kama unavyo jua mchaka mchaka wakulisongesha jambo la fashion bado unaendelea yaani siwezi kuliacha nishakula kiapo cha kuwaelimisha mambo kadha wa kadha kuhusiana na fashooooon, mitindoo, urembo nk!!!.

Wanawake na urembo wao bhana week iliopita tulikuwa na mada ya uoshaji wa nywele zako tukaelekezana mambo mengi mnoo, sasa furaidaiiiiii hiiii!! Nakusongezea kitu hiki hapa hivi ulisha wahi jiuliza au hata kusikia maji ya mchele yanaweza kukuza nywele zako sasa basi ungana nami mwanzo mpaka mwisho ili uweze kuelimika zaidii…

Tumeshazoe mara ohooo!! parachichi ina kuza nywele sjui mafuta fulani yanakuza nywele  mara kitunguu maji wee! Achana na yote hayo mwamba huyu hapa, hitaji lako sahihi kwasasa ni maji ya mchele upooo..

Wengi wenu mtakuwa mnajiuliza haswa kuwa kwani maji ya mchele ni yapi, yapoje, siunajua bwana wale washua tutakuwa kama tumewaacha mbali hivi, maji ya mchele yanatokana na mchele ukiuosha au kuuloweka yale maji yanayokuwa na rangi ya maziwa ndo maji ninayoyazungumzia mimi hapa.

Inashangaza eeeh! ndio na ina weza isiaminike lakini huo ndio ukweli, Maji ya mchele yana faida kubwa katika nywele una weza kuuliza kivipi na nani yamemsaidia, stori iko hivi, unaambiwa bwana kabila la Yao kutoka kijiji cha Huangluo  Nchini China ndilo kabila ambalo lina wanawake wenye nywele ndefu zaidi duniani, ambapo wanaweza kufunga nywele zao kama kiremba na ukiwauliza hii ndo siri ya mafanikio yao.

Baadhi ya wanawake hao wanaamini kutumia maji ya mchele kuoshea nywele zao huwafanya nywele zao kuwa ndefu zenye afya na kuto kupatwa kwa mvi mpaka kufikia miaka ya 80.

Haya shoga angu unaanzaje kupata mvi haswa ukiujua urembo na matumizi yake, kwa mataifa ya wenzetu maji ya mchele wananunua madukani kwa ajili tuu ya kupata urembo haya wewe mwenzangu na mie unapika kila siku lakini unaishia kuyamwaga tuu chini, zinduka now siku hizi kaulimbiu ni kila kitu kinafaida hadi takataka.

Ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua nini ufanye kupitia hayo maji ya mchelee..

Cha kufanya wakati unapika wali wako ongeza maji kidogo tofauti na yale uliyo yazoea kisha yakisha chemka na kuanza kuwa mazito na kubadilika rangi kuwa ya mchele punguza kwenye kibakuli na uyaache yapoe kabisa.

Angalizo jamani usijimwagie kichwani maji hayo ya kiwa ya moto usije uka babuka ukashindwa kupata matokeo mazuri bibieee, baada ya hapo yakisha poa paka kwenye nywele zako na ukae nayo kwa muda wa dakika 3-5 na uoshe kwa maji masafi.

Hii husaidia kukuza, kulinda nywele zisikatike na zilizo katika kurudi katika hali yake ya kawaida pamoja, ku ng’arisha nywele, kuondoa mba na miwasho kichwani nk. Weeeeeh! Unaona mambo hayoo

FAIDA ZA MAJI YA MCHELE KWENYE NYWELE

  • kulainisha nywele
  • yanajaza nywele kwa sababu ya Amino acid inayo patikana kwenye mchele.
  • kuimarisha nyewele & kufungua vitundu vya ngozi
  • kuondoa miwasho na mba kichwani
  • kujaza nywele
  • kufanya nywele zako ziwe na muonekano mzuri


JINSI YA KUAANDA MAJI YA MCHELE

Sasa hapa mrembo wangu wacha nikudadavulie kinaga ubaga mwanzo mpaka mwishoo maana hapo juu nilirashia mambo haya hapa

  • Andaa mchele wako robo kilo mchele aina yoyote ile usiwe tuu ule wa birian maana hamchelewi.
  • osha vizuri kisha weka kwenye sufuria
  • weka maji mengi kadri utakavyo kwenye mchele wako
  • Acha ya uchemke dakika10 kwa moto wa wa stani mpaka uone mchele unaanza kulainika
  • Chuja maji yako na weka kwenye kopo maji unayo ya chuja na ufunike vizuri  usiku mzima, asubuhi ongeza maji kikombe kimoja ili kupunguza nguvu.
  • Hifadhi maji yako kwenye friji kwa muda wa wiki mbili ya sipoteze ubora wake.

 NAMNA YA KUTUMIA MAJI YA MCHELE

  1. Osha nywele zako kwa shampoo kama kawaida hakikisha unasugua kichwa kizima mpaka nywele zitakate
  2. Fanya deep conditioning kwa dakika30
  3. Osha tena nywele zako na maji ya kawaida
  4. Kisha anzakupaka yale maji ya mchele kwenye nywele hakikisha yanasamba kichwa kizima hadi kwenye ngozi, na utulie ndani ya dakika3 mpka5 kisha ndio unoshe tena na ukimaliza zikaushe nywele zako lazima utaona utofauti tuu 

Najua kama ni kaprocess kidogo lakini siku zote mtaka lake hashindwi, kwanini kila siku wewe uwe unauliza wenzio unapaka dawa gani, unatumia mafuta gani kwanini usifanye ulichoelekezwa nawewe ukaona maajabu kuwa mwalimu kwa wengine, changamka sasa na ujue tuu maji ya mchele yanavitamins A,B,E na amino acid ambapo vitamin vyote hivyo vinafaida sana katika nywele zako.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags