Maisha ya marehemu Mohbad, muziki wake, kukamatwa na polisi, mafanikio, changamoto na kifo chake

Maisha ya marehemu Mohbad, muziki wake, kukamatwa na polisi, mafanikio, changamoto na kifo chake

Whats Up familia?, its another Friday tumekutana hapa kupeana mawili matatu ya kiburudani, i hope mko njema kabisa lakini kwa wale wenye matatizo mbalimbali mimi nawaombea ili muweze kuwa sawa.

Wanangu kama ilivyo kawaida chimbo letu hili ni kwa ajili ya masuala ya kiburudani, kama ambavyo huwa atuchagui burudani kutoka nchi gani, basi na katika hili la leo nikaona si vibaya tukiweza kushirikishana.

Kwanza kabisa kabla sijakimbia kwenye maandishi yangu napenda kuwapa pole mashabiki wote wa burudani ya muziki ambao mnatufatilia kupitia jarida letu pendwa la Mwananchi Scoop, pole yangu hii ni kuhusiana na msiba mkubwa ambao unakabili wanaburudai wa kumpoteza mwanamuziki na muandishi kutoka nchini Nigeria, MohBad.


Taarifa za kifo chake wengi walianza kuzipata Septemba 12, 2023, huku mswali ya kifo chake yakiwa mengi kuhusu mkali huyu wa muziki.

Kwanza kabisa naomba tujuzane mambo yanayomuhusu, kama ulikuwa hufahamu MohBad jina lake kamili ni Ilerioluwa Oladimeji Aloba, alizaliwa June 8, 1996 Ketu, Lagos, nchini Nigeria, yaani kwa hesabu za haraka amefariki akiwa na miaka 27.

Maisha yake ya muziki alikuwa akitambulika kama muimbaji na muandishi wa muziki, alianza kujulikana zaidi kuanzia mwaka 2019 hadi 2023 ambapo ndiyo mwaka aliyopoteza maisha yake.

MohBad mwaka 2019 alijiunga na label ya Naira Marley's Marlian Records, ambapo aliachana na label hiyo mwaka 2022. MohBad alitamba zaidi na kufahamika kwa hit songs zake kama vile "Ponmo, Feel Good", na "KPK (Ko Por Ke)".

Alitoa albamu yake ya kwanza ‘Light’, mwaka 2020, MohBad aliorodheshwa katika wasanii 21 bora wa Afrobeat wa Audiomack wa 2021, na 2022 alitoa wimbo wa ‘Peace’, uliyotayarishwa na Rexxie na kupelekea kuingia kwenye ‘chati’ za Turn Table 50 bora mwaka 2021 na 100 bora za mwaka 2022 na wimbo huo wa peace pia ulishika nafasi ya kwanza katika ‘chati’ ya muziki ya Apple Nigeria.

Kutokana na ukali wa ngoma zake alifanikiwa kuingia mara tatu kwenye tuzo za The Headies mwaka 2022, si hivyo tu mwaka 2021 aliweza kutajwa mara tano kwenye tuzo za The Beatz Awards.



Mafanikio kwake hayakuishia hapo hata baada ya kutoka kwenye label ya Marlian Record World aliweza kufanikiwa kutoa EP yake ya kwanza Juni 2023 iliyofahamika kama “Blessed”, akiwa chini ya label yake aliyoianzisha mwenyewe, inayofahamika kama Imolenization.

‘Blessed’ ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye Apple Music nchini Nigeria kwenye week ya kwanza ambayo ilitolewa, na mara tu baada ya kifo chake iliweza kuingia tena kwenye namba moja .

Kama ilivyo kawaida kwenye harakati za maisha kuna yale magumu ambayo watu hupitia ndivyo kwa MohBad Februari 2022, Shirika la Kitaifa la Utekelezaji wa Sheria ya Dawa za Kulevya (NDLEA) lilimkamata MohBad, Zinoleesky, na wenzake wanne nyumbani kwao Lekki, Lagos kwa kukutwa na dawa za kulevya ikiwemo bangi, lakini baadaye walifanikiwa kuachiwa huru.

Baada ya kutokea kwa kifo chake tuhuma nyingi zimekuwa zikimuendea aliyekuwa manager wake wa label ya Marlian Record World, Naira Marley's na Sam Larry kutokana na migogoro waliyokuwa nayo tangu aondoke kwenye label hiyo.

Ngoja nikusanue mtu wangu kuhusu tuhuma hizo, ipo hiviiii baada ya miaka miwili Mohbad alitangaza kuondoka kwenye label ya Marlian Records, hapo ndipo hekeheke zikaanza na ugomvi wa hapa na pale.

Tarehe 5 Oktoba 2022, MohBad alimshutumu mwimbaji Naira Marley, kwa kumshambulia na kusema kuwa aliamuru watu wampige baada ya kutangaza kuwa anataka kuanza kufanya kazi na manager mwingine katika masuala yake ya muziki.

Hata hivyo baada ya kifo cha MohBad, iliripotiwa kuwa kabla ya kupatwa na umauti alikuwa amepeleka malalamiko polisi Juni 2023, akidai kuwa ‘promota wa muziki anayeitwa "Sam Larry" na Naira Marley, walimvamia na kuharibu baadhi ya mali zake wakiwa na kundi la wanaume wasiyopungua 15 wakiwa na bunduki.

Kutokana na tuhuma hizo za Naira Marley amejikuta katika wakati mgumu nchini Nigeria ambapo nyimbo zake zimepigwa marufuku kupiga kwenye vituo vya redio na Television nchini humo huku akiwa amepoteza wafuasi wengi kwenye mtandao wa kijamii.

MohBad ameacha mke na mtoto mmoja wa kiume, mke wake anafahamika kama , Wunmi.

MohBad alifariki tarehe 12 Septemba 2023, akiwa na umri wa miaka 27 huku sababu ya kifo chake ikiwa haijawekwa wazi na kuzua utata mkubwa kwa baadhi ya mashabiki hasa suala la kuuzika mwili wake haraka bila uchunguzi.

Kutokana na hili maandamano ya amani yamekuwa yakiendelea nchini Nigeria yakiongozwa na wasanii kama Davido kutaka haki ya msanii huyo, ambaye kwa kibali cha polisi mwili wake ilibidi ufukuliwe kwa ajili ya uchunguzi wa kifo chake kama ambavyo mashabiki wanataka.

Bado unaweza kuendelea kujiburudisha na ngoma za MohBad kama vile “Backside”, “Weekend”, “Tiff”, “Hallelujah”, “Ronaldo”, “Feel Good” na “Peace”.

Hadi kufika hapo mimi sina cha ziada zaidi ya kusema RIP MohBad. Tchaooo wasomaji wangu wa nguvu tukutane tena Furahii deii ijayo kama tulivyofanya leo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post