Mafuriko yaigharimu Pakistan

Mafuriko yaigharimu Pakistan

Hii ni kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mipango, AhsanIqbal inasema makadirio ya awali yanaonesha mafuriko makubwa yaliyoikumba Nchi hiyo, yamesababisha uharibifu wa karibu Tsh. Trilioni 23.

Tayari Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetoa msaada wa Tsh. Trilioni 2.5 kwaajili ya kukabiliana na madhara ya mafuriko ambapo kwa mujibu wa Serikali, theluthi moja ya Nchi imeharibiwa vibaya

Hata hivyo Mvua za Masika zinazonyesha zimesababisha vifo vya Watu 1,136 na kuathiri Maisha ya Watu milioni 33 ambao ni zaidi ya 15% ya idadi ya Watu Nchini humo. Pia, zimesomba Barabara, Mazao, Nyumba, Madaraja na Miundombinu mingine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags