Madhara ya utoaji wa mimba

Madhara ya utoaji wa mimba

Hellow! Watu wetu wa nguvu kama kawaida yetu katika afya leo tumekusogezea mada nzito. Tunajua unajua madhara ya utoaji wa mimba lakini tunataka kukujuza zaidi kuhusiana na tatizo hili ili kudhibiti janga hili.

Kabla hujafikiria kutoa mimba ni muhimu kufahamu matokeo mabaya kiafya yanayoweza kujitokeza siku za mbele baada ya kufanya kitendo hichi, hasa kwenye suala zima la uzazi.

NINI KINATOKEA BAADA YA KUTOA MIMBA?

Wanawake wengi hupata dalili hizi siku chache baada ya kutoa mimba, dalili ambazo zinaweza kuchukua mpaka siku 21 kuisha

  1. Kutokwa damu kwa wiki 2 mpaka 4
  2. Maumivu ya nyonga
  3. Mwili kukosa nguvu na kusinzia ovyo
  4. Kutapika na kizunguzungu

MADHARA MAKUBWA YANAYOWEZA KUJITOKEZA BAADA YA KUTOA MIMBA NI PAMOJA NA:

. Majeraha kwenye mlango wa kizazi na kizazi

. Kutokwa damu kupita kiasi mpaka kuishiwa damu

. Mimba kushindwa kutoka yote (incomplete abortion) na hivyo kuhitaji upasuaji mwingine

. Maambukizi sugu kwenye via vya uzazi (PID)

. Makovu kwenye tumbo la uzazi

. Kufanyika kwa mashimo ndani ya kizazi

. Mgonjwa kufariki

MADHARA YA MUDA MREFU BAADA YA KUTOA MIMBA

. Kujifungua mtoto kabla ya muda wake kutimia (pre-term delivery)

. Kutoa mimba husababisha kulegea kwa mlango wa kizazi na hivyo kuongeza hatari ya mimba zijazo kutoka ama kujifungua kabla ya wakati yaani chini ya week 37.

. Endapo mtoto atazaliwa chini ya muda wa week 37 anaweza kupata madhara ya kiafya kama matatizo ya ubongo.

. Saratani ya matiti: Tafiti zinasema kwamba kutoa mimba kunaongeza hatari ya mwanamke kupata saratani ya matiti.

. Kuugua magonjwa sugu kama chlamydia na PID

. Kupata magonjwa ya akili: Tafiti zinasema kwamba wanawake wengi hupata matatizo ya akili baada ya kutoa mimba na dalili kama

  • Kujutia kutoa mimba
  • Sonona na msongo mkubwa wa mawazo
  • Kupata wasiwasi kama je watashika tena ujauzito mwingine
  • Kuona aibu na kujihisi wakosaji
  • Kupata mawazo ya kujiua

Kama ulitoa mimba na unaanza kupata dalili hizi hapa juu, chukua hatua mapema, onana na mtaalamu wa afya ya akili kupata ushauri wa kina.

KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO KWA SIKU ZA BAADAYE BAADA YA KUTOA MIMBA

1.Kutokana na athari ya magonjwa kama PID kwenye kizazi na mirija, inaweza kupelekea mwanamke kushindwa kushika mimba kwa siku za baadaye.

2.Kwa mwanamke aliyetolewa mimba hospitali kutokana na changamoto za kiafya, hatari ya kukosa mimba kwa siku zijazo ni kubwa hasa kama mwanamke husika ana changamoto za kisukari, magonjwa ya figo, ini, moyo na mapafu na kuchanika kwa kizazi.

3.Kushindwa kushiriki tendo la ndoa ipasavyo. 

BAADA YA KUTOA MIMBA WANAWAKE HUWEZA KUPATA CHANGAMOTO KWENYE TENDO LA NDOA KUTOKANA NA; 

  1. Uke kuwa mkavu sana
  2. Kupungua kwa hamu ya kushiriki tendo
  3. Kushindwa kufika kileleni na
  4. Maumivu makali wakati wa tendo.

Haya sasa,katika jarida lijalo tutazungumzia ugonjwa wa PID, ambao  moja ya visababishi vyake ni utoaji mimba, pia ni tatizo ambalo linaweza kukusababishia madhara makubwa.

Imeandaliwa na Mark Lewis.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags