Madhara ya unywaji wa kahawa kupitiliza unapokuwa mahala pa kazi

Madhara ya unywaji wa kahawa kupitiliza unapokuwa mahala pa kazi

Na Glorian Sulle

Moja ya kinywaji ambacho hupendelewa haswa na wafanyakazi wengi katika maofisi mbalimbali ‘kahawa’ ndio namba moja, hii ni kutokana na madai kuwa inawasaidia kuondokana na uchovu, usingizi na kuwaweka sawa.

Waswahili wanasema kizuri hakikosi kasoro, basi Mwananchi Scoop leo inakuletea Makala iliyojikita kuangalia madhara ya unywaji wa kahawa kupitiliza haswa maeneo ya kazini.

Kwa mtazamo wa kitaalamu matumizi ya kahawa yaliyopitiliza ni hatari kwa afya.

Akizungumza katika mahojiano na Mwananchi Scoop Aprili 26, 2024 mtaalamu wa afya ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Clecensia Massawe amesema kahawa ina kafeini ambayo huupa mwili nguvu zaidi ya uhalisia wake.

“Kama umechoka, ukinywa kahawa unajiona umepata nguvu na unaweza kuendelea na kazi, hiyo ni kwa sababu ya kafeini” amesema

Dk Clecensia anasema hatari ya kinywaji hicho ni mtu anapotumia kupita kiasi na kutengeneza uraibu.

“Unakuta mtu anakunywa kahawa kama chai, kila wakati anachukua anakunywa hili ni tatizo na litamwathiri na miongoni mwa athari hizo ni pamoja na kuuzidishia mwili kiwango cha kufanya kazi na kupunguza muda wa kulala” amesema Dk Clecensia

Hata hivyo alimalizia kwa kuwasisitizia baadhi ya watu pamoja na wafanyakazi wnaaopendelea kunywa kahawa kwa wingi kuangalia kiwango cha kafeini kabla kutumia kahawa hiyo.

Aidha hatukuishia hapo tulipata wasaha wa kuzungumza na mtaalamu wa magonjwa ya binadamu, Profesa Andrea Pembe ambaye ameweka wazi matumizi ya kahawa kupitiliza husababisha shinikizo la juu la damu.

“Kafeini iliyopo katika kahawa inasababisha moyo kwenda kasi, hivyo kuhatarisha maisha ya watu wenye presha iliyo juu kuliko kawaida (hypertension)” anasema

Madhara mengine yanayoletwa na kinywaji hicho ni ‘utegemezi’

‘Utegemezi’ ni hali ya kuwa na uraibu wa kupindukia hali ya kuona huwezi kuishi au kufanya jambo lolote mpaka utakapopata kinywaji hicho.

Historia ya kahawa

Kahawa iligunduliwa karne ya 9, na mchungaji wa mbuzi aitwaye Kaldi, kutoka nchini Yemen huku nchi hiyo ilitajwa kuwa ya kwanza kuchuma mbegu ya kahawa katika karne ya 14 na kutengeneza kinywaji kinachotumika hadi leo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags