Madee atangaza kuacha muziki

Madee atangaza kuacha muziki

Mwanamuziki mkongwe wa Hip Hop, Hamadi Ally Seneda maarufu kama Madeeali ametangaza rasmi kuachana na muziki baada ya kuufanya kwa miaka 20.

Kupitia mitandao yake ya kijamii mwamba huyo aliyesumbua Airwaves na hits kama Kazi yake Mola, Hela na zingine kibao ametoa taarifa hiyo akisema.

“Umri wangu umekwenda sana, namshkuru Mungu kwa huu muda alionipa, kwasababu nimeshuhudia marafiki wengi sana hawakubahatika kufikia zaidi ya miaka 40” alisema Madeeali.

Mwisho akasema kuwa anajuta kuwa maarufu kwasababu umemchelewesha kuja kwenye maisha mengine “umaarufu mbaya sana, nimeamua kuacha yote, naanza na hili, staki tena muziki na mengineyo” alisema mkali huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags