Maandamano yazuka baada ya ajali ya Treni, Ugiriki

Maandamano yazuka baada ya ajali ya Treni, Ugiriki

Maandamano yamezuka nchini Ugiriki kufuatia na ajali ya reli iliyosababisha vifo vya watu 43, huku wengi wakiiona kama ajali iliyokuwa ikisubiriwa kutokea.

Waandamanaji hao walikabiliana na polisi nje ya makao makuu ya Hellenic Train mjini Athens, kampuni inayohusika na utengenezaji wa miundombinu ya reli nchini humo.

Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa kote nchini kufuatia kisa hicho, ambapo treini ya abiria iligongana na treni ya mizigo na kusababisha mabehewa ya mbele kuwaka moto.

Abiria 350 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walikuwa wanafunzi wenye umri wa miaka 20 waliokuwa wakirejea Thessaloniki baada ya wikendi ndefu kusherehekea Kwaresima ya Orthodox ya Ugiriki.

Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis alisema "makosa mabaya ya kibinadamu ndio yalisababisha maafa hayo. Msimamizi wa kituo cha Larissa amefunguliwa mashtaka ya kuua bila kukusudia. Na Serikali ya nchi hiyo imesema uchunguzi huru utatoa maelezo kamili.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags