Maana tofauti ya upendo katika mahusiano

Maana tofauti ya upendo katika mahusiano

Hellow! Niaje mtu wangu wa nguvu, leo kwenye mahusiano bwana nakusogezea mada moja konki ambayo itakupa uelewa kuhusiana na maswala mazima ya upendo katika mahusiano. Najua ntakuwa kama nimekuchanganya ila ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua Zaidi. 

Ni jambo la kawaida kujiuliza kama unampenda fulani au kama fulani anakupenda, wengi hujikuta wakipata maana tofauti, kwa  uzoefu wangu unanifanya niamini kuna maana tofauti kuu 3 zinazojitokeza miongoni mwetu wakati wa kutafakari swala la upendo katika mapenzi/mahusiano.

Haya sasa ungana nami kujua maana tofauti za upendo katika mahusiano, kwa mada hii itakusaidia kabisa kujua watu wanavyotafsiri tofauti neon upendo katika mahusiano…. 

  • Kujali

Kuna wanaoamini kuwa kujali tuu inatosha kuonyesha kuwa unampenda fulani, au fulani kuonyesha anakujali basi hiyo ndio maana halisi ya upendo. Wengi hujikuta wakitumia muda mwingi kutafuta zawadi na surprises za ‘nguvu’ kama sehemu kuu ya kuonyesha upendo wao.

Aina hii ya upendo inahusika sana hasa kwa watu waliopo mashuleni na vyuoni. Wengi wanaoamini maana hii ya upendo, husisitiza sana kuogopwa/kunyenyekewa kama sehemu ya kuonyeshwa kuwa nao wanapendwa.

  • Kujitoa kafara

Katika maana hii, upendo ni swala la jinsi gani unavyojitoa kwa mwingine ili kuona anakuwa na furaha na anajihisi kuwa salama kutokana na uwepo wako.

La msingi katika aina hii ya upendo ni kupenda kumfahamu vema mwenzi wako, kujua shida zake, na ndoto zake, na kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha anaona uwepesi katika shida zake, na kuwa anakuwa na matumaini ya kuwa ndoto zake zitatimia. Upendo wa namna hii huwa na subira, na huonekana zaidi kwa waliokomaa kifikra, na wenye kujiheshimu wao wenyewe.

  • Kuvutia na mtu

Kwa wengine upendo ni namna gani wanavyovutiwa kimapenzi na mtu husika, au vile wanavyojisikia kuwa salama mbele ya mtu fulani.  Utakuta mtu anasema anampenda kaka/dada fulani kwakuwa tuu amevutiwa na uhodari wa mtu husika katika masomo, kujiheshimu, sifa au umaarufu alionao mhusika. Na kwa upande mwingine, mtu anaweza kuvutia kwa uzuri wa sura au umbile  lake.

Aidha kutokana na mvuto wa hisia kama hizo na wakati mwingine hisia hizi za mvuto huwa kali sana, basi mtu akadhani hiyo ndiyo maana halisi ya Upendo.

Naomba tuelewane kidogo kuwa siku zote upendo ni jambo lisilo na ubinafsi, haliangali nafsi yako inataka kunufaika kiasi gani, bali unataka kuinufaisha nafsi ya mwingine kwa kiwango gani. 

Hivyo kwa upande wetu, maana ya upendo tunayoipendekeza ni kujitoa kafara, kama tulivyoielezea hapo juu. All in all inakupasa utambue kuwa upendo pekee hautoshi kujenga mahusiano yenye furaha na yenye kudumu. 

Aloooooh! Kumbe kwenye mahusiano kuna mambo mengi hivi na hamsemi watu mnasiri sana jamani, basi bwana kwa mada za mahusiano mbalimbali usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags