Maambukizi 60 ya janga la  kipindupindu yaripotiwa, Kenya

Maambukizi 60 ya janga la kipindupindu yaripotiwa, Kenya

Kaunti 6 nchini Kenya, ukiwemo mji mkuu Nairobi, zinakabiliwa na janga la kipindupindu. Takriban maambukizi 60 yameripotiwa huku watu 13 wakilazwa hospitalini.

Hii ni kulingana na taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Afya ambayo imebaini kuwa chanzo cha mripuko wa ugonjwa huo ilikuwa karamu ya harusi katika Kaunti ya Kiambu, takriban kilomita kumi kaskazini mwa mji mkuu Nairobi.

Ukame unaolikumba taifa hilo lenye watu milioni 50, unaweza kuzidisha janga hilo. Januari mwaka 2016, Wasomali wasiopungua 10 walikufa kwa kipindupindu na wengine 1,000 waliugua ugonjwa huo katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, ambayo ni kubwa zaidi duniani.

Kipindupindu ni ugonjwa hatari unaoambukia, na usipotibiwa haraka unaweza kusababisha kifo ndani ya muda mfupi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags