Najua ni vigumu kueleza kinagaubaga maana halisi ya neno urembo ila naweza kusema kuwa urembo ni utumiaji wa mapambo, manukato, marashi, uturi, mavazi na rangi ili kupendeza na kuongeza nakshi na umaridadi katika mwonekano.
Leo tuna kitu cha tofauti kwenye segment yetu, maajabu na faida mbalimbali za manjano kwenye ngozi yako.
Kwanza kabisa manjano ni kiungo kinachotokana na mti uitwao Curcuma longa, mti huu unapatikana sana Kusini mwa bara la Asia, kiungo hiki kinatumiwa kwa namna nyingi.
Hata hivyo siku hizi mambo yamebadilika manjano ambayo yalikuwa ni kiungo muhimu katika chakula sasa hivi kimekuwa kiungo muhimu katika ngozi, yaani urembo wako unakuwa haujakamilika kabisa bila kutumia manjano.
Ieleweke kuwa manjano mabichi ambayo hayajazimuliwa na sembe ndio mazuri hivyo epuka kutumia manjano yaliyochanganywa tayari na sembe ujue kutofautisha manjano ya chakula naya urembo.
Manjano yanaweza kukusaidia katika urembo kutibu chunusi, kutokana na tabia yake ya kupambana na bacteria manjano yanauwezo wa kukausha chunusi hasa zile zinazotokana na maambukizi ya bacteria na kufanya ngozi kuwa soft kabisa na kuwa na nuru.
Sasa kwa mwenye ngozi ya mafuta unachanganya manjano na maji ya waridi na wale wenye ngozi kavu unachanganya manjani hayo na maziwa fresh kisha unapaka usoni kwa nusu saa kisha unaosha na maji ya kawaida au unaweza ukachanganya manjano na Asali ukapaka mwili mzima kwa dakika kadhaa upendavyo wewe kwa kila siku lazima matokeo ya ngozi yako utayaona mazuri.
Manjano yanang’arisha ngozi, kama ujui manjano yanatabia ya kutoa weusi kwenye ngozi unaotokana na ‘crimu’, kuungua na jua au kufubaa kwa ngozi, unachotakiwa kufanya changanya manjano na maji ya waridi kisha sugua sehemu iliyoathirika.
Pia manjano inapunguza mafuta kwa wenye ngozi yenye mafuta pia usaidia sana kupunguza uzalishaji wa mafuta hapa utashangaa unachotakiwa kufanya ni kunywa ‘glasi’ moja ya mchanganyiko wa maji na manjano angalau mara mbili kwa wiki.
Licha ya hivyo manjano upunguza kasi ya ngozi kuzeeka baada ya matumizi mengi ya vipondozi (make up), fanya mazoea na ujitahidi kila mwisho wa wiki uwe unausugua uso wako kwa manjano angalau mara moja maana manjano haya usaidia ngozi isichoke haraka na nuru yangozi yako kudumu muda wote.
Kufika hapo nadhani tumewekana sawa kuhusu matumizi na faida za manjano sasa nitakushangaa msichana wa kileo ukapitwa na urembo huu wa manjano hakikisha tu unafuata maelekezo jinsi ya kutumia manjano.
Nikwambie tu ni vyema tukaonana tena next week undelee kupata usicho kijua kwenye Urembo na Fashion.
Leave a Reply