Lupita Nyongo kuitangaza Zanzibar

Lupita Nyongo kuitangaza Zanzibar

Whats up my beautiful people! Its another time bila kupoa tunakusogezea stori moto moto. Ebwana eeenh!! Tanzania ndo inazidi kuchukua nafasi ulimwenguni kuwa miongoni mwa nchi yenye vivutio vizuri vya utalii, pongezi za dhati ziende kwa uongozi wa awamu ya 6 kwa kuitangaza vyema sekta ya utalii kupitia filamu ya Royal Tour.

Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vyenye vivutio vingi vya utalii, basi bhana muigizaji wa filamu maarufu kwa jina la Lupita Nyong'o ambaye ni mzaliwa wa Kenya na kwa sasa anaishi katika mataifa ya Mexico na Marekani, kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost video akiwa kisiwani Zanzibar na kushiriki mchezo wa kuogelea kwa kujirusha kwenye maji na vijana wa Forodhani Garden.

Kupitia video hiyo Lupita alipendezwa na aina hiyo ya uogeleaji, pia alimshukuru Jamal ambaye ni kiongozi wa michezo hiyo Forodhani kwa kumualika kwa kusema “This is amaizing, thank you Jamal ,welcome Zanzibar.”

Hii ni baada ya vijana hao kumualika Lupita kutembelea Zanzibar miezi kadhaa iliyopita ambapo kupitia ukurasa wa Instagram wa Jamal, video ilipostiwa wakiwa wanaruka majini huku wakishikilia picha ya nguli huyo wa filamu ya Black Panther huku wakisikika wakisema "Lupita, welcome to Zanzibar."

Alooooh! Vijana wa eneo hilo wamefanikiwa kuitangaza Zanzibar duniani kwa aina hiyo ya uogeleaji na kutoa ushawishi kwa mastaa wa kubwa kufika kisiwa cha karafuu. Shusha comment yako ukitueleza unatumia vipi fursa ya utalii iliyopo katika eneo lako kujiajiri?Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post