Lupita Nyong o aunga mkono maandamano Kenya

Lupita Nyong o aunga mkono maandamano Kenya

Mwigizaji kutoka Marekani mwenye asili ya Kenya Lupita Nyongo amelipongeza kundi la vijana la ‘Gen Z’ na wananchi wote nchini humo kwa kuchukua uamuzi wa kuandamana kupinga Muswada mpya wa fedha wa 2024.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nyongo ame-share ujumbe akiwashukuru Wakenya kwa ujumla kujumuika kutetea haki zao huku akiitaka Serikali ya Kenya kusikiliza ombi la wananchi wao na kulifanyia kazi.

“Ninawasalimu Wakenya na ninawashukuru sana kwa kujumuika pamoja kwa njia ya ajabu ili kusimama dhidi ya mswada wa kifedha ambao haupo sawa wa 2024 na pia kutetea na kukuza haki ya kidemokrasia ya watu wa Kenya.

Nina huzuni kubwa kwamba baadhi ya watu wamepoteza maisha katika mchakato huo kwa maoni yangu naomba serikali ya Kenya iliunganishe tena Taifa hilo kwa kusikiliza na kushughulikia matatizo yanayo jitokeza” ameanadika Nyongo

Mkali huyo wa ‘Black Panther’ amewahi kuonekana katika filamu kama ‘Queen of Katwe’, ‘12 Years a Slave’, ‘A Quiet Place: Day One’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags