Luisa atimiza ndoto ya kutembea nchi zote duniani

Luisa atimiza ndoto ya kutembea nchi zote duniani

Bibi wa miaka 79 anayefahamika kwa jina la Luisa Yu mzaliwa wa Ufilipino,ametimiza ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani kama alivyokuwa akitamani.

Bibi huyo amekuwa na tabia ya kutembea kwenye nchi mbalimbali kila mara akipata nafasi, kutokana na kuvutiwa na mandhari nzuri za sehemu tofauti tofauti anazoziona kwenye movie.

Wakati akifurahia kutimiza ndoto yake hiyo bibi huyo anawashauri watu wenye ndoto kama yake kuitimiza kila wakipata nafasi bila kuogopa, anawataka kuchangamka kila wapatapo fursa ya kusafiri. Nchi ya mwisho ambayo ni ya 193 aliyoitimisha nayo ni Serbi.

Alipotembelea Tanzania alifika maeneo mbalimbali kama vile Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Zanzibar


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post