Loyal ya Chris Brown yaibukia TikTok

Loyal ya Chris Brown yaibukia TikTok

Ngoma ya Loyal ya mkali Chris Brown yaibukia kwenye mtandao wa TikTok ambako watu mbalimbali wamekuwa wakitumia kuchapisha video zao.

Ngoma hiyo ambayo ilitoka Machi 24, 2014 huku ikiwa na matoleo mawili ambapo toleo la kwanza akiwashirikisha wakali kama Lil Wayne pamoja na Tyga huku toleo la pili akimuongeza French Montana na kumuondoa Tyga ilishika nafasi mbalimbali za juu kweye chati maarufu za muziki zinazofahamika kama BillBoard hot 100.

Ngoma hiyo ambayo ilibeba nafasi nyingi za juu ilimrudisha kwenye ramani baada kimya cha muda mrefu Chris Brown na kupeleka mkali huyo kuja na kazi kubwa za Sanaa zilizofanya vizuri ikiwemo albamu yake ya Fan Of A Fan aliyoshirikiana na Rapa Tyga.

Loyal ni miongoni mwa ngoma kubwa na maarufu zaidi duniani kutoka kwa Breezy, ambapo video yake imetazamwa zaidi ya mara Billion 1.4 huko kwenye mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags