Linex ampa makavu Baba Levo

Linex ampa makavu Baba Levo

Mambo ni moto mambo ni fire leo kwenye gumzo mitamdaoni bwana kumewaka, Staa wa muziki nchini Tanzania Linex Sunday maarufu kama Mjeda amemtolea uvivu msanii mwenzie  Baba Levo baada ya kuongelea maisha yake mara kwa mara kwenye vyombo vya habari

Kupitia ukurasa wake wa instagam Linex alifunguka na kusema “Baba Levo achaga kuongea ongea mambo zangu au past zangu kwenye radio plzzz live me alone bro, na kama kuna sehemu nilikukosea nisamehe namaanisha kuna vitu kibao vya kuongelea au kuzungumza usinifanye content plz nina maisha nje ya kujulikana” amesema Linex

 Linex na Baba levo ni marafiki wa muda mrefu, Baba levo alishawahi kukiri kusaidiwa na Linex wakati alipokuja Dar es salaam kuja kupambania kipaji chake cha muziki.

Hata hivyo Baba levo amekuwa akifunguka matukio waliokuwa wakiyapitia miaka ya nyuma,   Si hivyo tuu Baba Levo amekua akilitaja jina la Linex kwenye mifano mbalimbali  afanyapo mahojiano kwenye vyombo vya habari jambo ambalo limemfanya Linex akwazike.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags