Lil Uzi Vert miaka mitatu chini ya uangalizi

Lil Uzi Vert miaka mitatu chini ya uangalizi

Rapper kutoka nchini America Lil Uzi Vert ameamua kusaini hati ya makubaliano ya kukubali kosa katika kesi ya jinai iliyomkabili ikimhusisha mpenzi wake wa zamani na msanii mwenzake aitwaye Saint jhn.

Aidha baada ya kukubali kosa akahukumiwa miaka 3 chini ya uangalizi, mwaka 1 wa kuhudhuria matibabu yanayohusu afya ya akili na uraibu, anatakiwa kupata ushauri nasaha kwa wiki 52 pamoja na kulipa fidia, lakini pia kutofanya kosa lolote la jinai kwa miaka 10

Nikukumbushe tu kuwa kosa lilifanyika mnamo  julai 2021 ambapo mpenzi wake wa zamani brittany byrd alikuwa na mazungumzo na saint jhn huko west hollywood. alifika eneo walilipo na akatoa bastola na kufanya vurugu.brittany alienda kufungua kesi akidai uzi alimwekea bastola tumboni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags