Inafahamika kuwa kwenye jamii kumekuwa aina mbalimbali ya matamasha ikiwemo ya kiburudani, dini, biashara, ya kitamaduni na mengine mengi, japo yapo yale ambayo Dunia nzima huadhimisha na ambayo husherekewa na nchi husika.
Umewahi kufahamu kuwa kuna tamasha la watu waliozaliwa mapacha? Kama una pacha wako ama ulikuwa ufahamu jambo hili basi tambua kuwa kila mwaka mwezi Agosti mapacha kutoka nchi mbalimbali Duniani hukutana Twinsburg, Ohio kwa ajili kusherekea kuzaliwa mapacha.
Week ya kwanza ya mwezi Agosti kuanzia tarehe 4-6 huwakutanisha zaidi ya watu 2000 waliozaliwa mapacha kutoka mataifa mbalimbali kama vile Brazili, Australia, Ghana, Nigeria, Kanada, New Zealand, Ufaransa, Italia, Uingereza, Ubelgiji, Ujerumani, India, Japan na China kwa ajili ya kujumuika pamoja.
Katika tamasha hilo familia mbalimbali hujumuika kwa pamoja ikiwemo wazee kwa watoto ambao huanza siku hiyo kwa maandamano na gwaride jiji zima mbapo wakati matukio yote hayo wakati yakiendelea hurushwa moja kwa moja kwenye Television ya Taifa, huku mapacha hao wakiwa wamevalia mavazi ya kufanana.
Leave a Reply