Lifahamu Gereza La Hiari Kwa Mwenye Strees

Lifahamu Gereza La Hiari Kwa Mwenye Strees

Msongo wa mawazo, ni kawaida katika maisha ya kila siku, lakini jambo hilo likiwa endelevu linaweza kukuharibia mfumo mzima wa maisha na kujikuta ukiingia katika njia isiyo sahihi.

Korea Kusini, kuna kituo kinachofanana na gereza kiitwacho ‘Prison Inside Me’ ambacho mtu anakwenda kwa hiari kwa ajili ya kuondokana na msongo wa mawazo, kuchoka kisaikolojia (burnout), na matatizo ya maisha ya kisasa.

Mtu atakaye kwenda katika gereza hilo atajifungia kwa siku moja au zaidi katika chumba kidogo kifananacho na selo akiwa hana simu, intaneti, wala mawasiliano ya nje.



Endapo utapendelea kwenda katika gereza hilo utatakiwa kulipia ambapo itataegemea na muda wa kukaa ambapo saa 24 inagharimu dola 90 sawa na Laki Mbili, saa 48 dola 146 sawa na Laki Tatu, na wiki nzima inagharimu dola 470 sawa na Sh1.2 milion.

Ukiwa katika gereza hilo hakuna adhabu lakini pia utakula chakula ukitakacho pamoja na kufanya mazoezi ya kupumua pamoja na kuandika.



Kituo hiki kimekuwa maarufu sana Korea Kusini hasa kwa watu wanaotafuta utulivu ambapo tangu kufunguliwa kwake mwaka 2013, zaidi ya watu 2,000 wamehudhuria programu hio.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags