Leokadia Amanyisye: Biashara ya ususi imebadilisha maisha yangu chuoni

Leokadia Amanyisye: Biashara ya ususi imebadilisha maisha yangu chuoni

“Ninafanya biashara ya ususi yaani kusuka watu nywele za aina mbalimbali, hakika kazi hii imenisadia katika mahitaji mbalimbali ya hapa chuoni, hata hivyo ninazo ndoto za kuja kuwa mwanajeshi nasubiri nimalize chuo nikajaribu bahati yangu,”

Hiyo ni kauli ya Leokadia Amanyisye mwanafunzi katika Chuo cha Tumaini Campus ya Dar es Salaam (Tudarco) anayechukua masomo ya Sheria (LLB) ngazi ya degree.

Akizungumza na mwandishi wa MwananchiScoop, Amanyisye anasema anajishughulisha na biashara ya ususi, biashara ambayo imemsaidia kuweza kujikimu na maisha ya chuoni pamoja na mtaani.

Anasema anaipenda biashara hiyo kwa sabbau ni kipaji alichojaaliwa na Mungu hivyo anapaswa kukitumia ipasavyo kwa kujiingizia kipato na kuwapunguzia mzigo wazazi wake katika utoaji wa mahitaji mbalimbali.

Mwanadada huyo anafunguka kuwa aliamua kujikita zaidi katika baishara hiyo kutokana na ugumu wa maisha ya chuo hali iliyosababishiwa na kutokuwa na mkopo yaani kwa jina maarufu no boom.

“Mimi sikuwa na mkopo na ilikuwa ngumu mimi kuomba hela kwa mzazi kila siku na ukizingatia ni binti mkubwa tu na kipaji cha kusuka nilikuwa nacho, niliamua kuanza kusuka ili niweze kujipatia hela na kuacha kuwa tegemezi kwa wazazi wangu.

 

“Sikutegemea kama mambo yangebadirika baada ya uamuzi wangu huo lakini ndicho kilichotokea niliweza kupata fedha na kuna wakati nilijilaumu nilikuwa nasubiri nini,” anasema

Hata hivyo Amanyisye anasema kipaji cha kusuka kipo kwenye familia yao na shangazi yake anayejulikana kwa jina la Sarah ndio mwalimu wake aliyemfundisha kusuka watu nywele.

“Niliamua kufanya biashara hii kama fursa badala ya kusuka tu marafiki zangu bure nikaamua wawe kama wateja wangu, ushauri huu nilipewa na aliyekuwa Cr wa darasa, Innocent Munuo, rafiki yangu Kareem Pembe kutoka IFM pamoja na rafiki yangu wa karibu  Halifa  Halifa.

“Msisitizo niliopata kwao ulikuwa ni mchango mkubwa kwa sababu nilikuwa naon aibu kwanza kuwadai pesa rafiki zangu na wakati mwingine nilikuwa nasema siwezi kufanya hivyo, ila walinitia moyo na kuniambia nitumie kipaji change vizuri,” anasema

Atamani kuwa mwanajeshi

Amanyisye anasema licha ya kufanya biashara ya kusuka lakini anatamani kuwa mwanajeshi kwani ni kazi anayoipenda kuifanya katika maisha yake.

“Napenda kuwa mwanajeshi(role model wangu ni Shangazi yangu ni mwanajeshi anaitwa Dorothea Mangazini), nimekua nikitamani kuwa kama yeye tangu nipo mdogo, amekuwa akini inspire sana katika kila kitu kuhusu jeshini japokuwa wengi wanaongelea kama sehemu ya mateso.

 

“Niwaambie tu vijana wenzangu hakuna kazi rahisi kila kitu ili ukiweze lazima kwanza ukipende na kisha ukifanye kwa uaminifu na bidi, ukiweza kuyatimiza hayo basi utaona kazi ni rahisi mimi najua kwa uwezo wa mwenyezi Mungu ndoto zangu zitatimia,” anasema

Hata hivyo anasema anaipenda kazi ya uwanajeshi kwa sababu inamfanya mtu kuwa mkakamavu, jasiri, mwadilifu, mzalendo na kuipenda nchi yake.

Changamoto katika biashara zake

Anasema moja ya changamoto katika biashara yake ya ususi ni muda kwani umekuwa ukiingilia na wa masomo yake ya darasani.

“Kuna muda unahitajika darasani na muda huo huo unahitajika kwa mteja hii changamoto ndio kubwa zaidi ukiwa unasoma, na kwa sababu elimu ndo kipaombele cha kwanza unaacha wateja na kwenda darasai,”anasema

Aidha anasisitiza kuwa fedha anazozipata kupitia ususi zimemuwezesha kuondoka nyumbani na kujitegemea na kujikumu mahitaji yake madogo madogo bila ya kumtegemea mzazi.

Hata hivyo mwanadada huyo amewataka vijana wenzake kuamini katika kile anachokiwaza kuwa kinaweza kumuingizia kipato endapo tu atakifanyia kazi.

“Wengi wanayomawazo ya biashara ila kuamua kufanya ndio inakuwa changamoto, hivyo basi waamini hicho wanachokiwafanya na kukifanyia kazi,” anasema

 

Kitu anachokipenda

Anasema kitu kingine anachokipenda ni kusikiliza muziki pamoja na kutunza maua.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post