Leo Waziri Pindi Chana kwenye Mirabaha

Leo Waziri Pindi Chana kwenye Mirabaha

                  

Ofisi ya Haki Miliki Tanzania inatarajia kutoa mgao wa mirabaha kwa wasanii nchini. Huku waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo   Dkt. Pindi Chana, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ugawaji wa stakihi hizo.

Mirabaha hiyo inatokana na makusanyo kutoka sehemu mbalimbali ambako kazi za wasanii Nchini zinatumika kibiashara kama vituo vya redio na Tv na kadhalika.

Huku wasanii na watayarishaji wa muziki waliotajwa kuhudhuria katika tukio hilo akiwemo Diamond, Lamata, Harmonize, Alikiba, Profers J, Shilole, Mobetto, Wema, Joti, Kontawa,  Christina Shusho, Mzee Yusuph Mkojani, Makabila na wengineo.

Ikumbukwe tu Meneja Usajili na Kumbukumbu wa COSOTA, Philemone Kilaka hivi karibuni alithibitisha kuwa ofisi hiyo itatoa stahiki ya kila msanii aliyestahili kupata Mirabaha kwa mwaka 2022.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags