Lebron James na mpango wa kustaafu kucheza kikapu

Lebron James na mpango wa kustaafu kucheza kikapu

Katika tetesi za hapa na pale kwenye michezo inadaiwa nyota wa Los Angeles Lakers  anafikiria kustaafu baada ya timu yake kupoteza kwa michezo 4-0 dhidi ya Denver Nuggets  katika fainali za ukanda wa magharibi kwenye ligi ya kikapu ya NBA. 

Taarifa zinadai kuwa James aliyecheza NBA kwa misimu 20 amesema anahitaji muda kutafakari kama atarejea uwanjani kuendelea kucheza msimu ujao wa 2023/24, licha ya kuwa bado ana mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Dola Milioni 97  ni sawa na Bilioni 229 za kitanzania.

Duh! Una yapi ya kumsanua mwamba huyo kutokana na uamuzi wake, dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags