Laini zisizohakikiwa kuzimwa Januari 31, 2023

Laini zisizohakikiwa kuzimwa Januari 31, 2023

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tamko la kuzifunga laini zote ambazo hazikuhakikiwa. Mamlaka hiyo imeeleza maamuzi hayo yana lengo la kumlinda mtumiaji dhidi ya uhalifu wa mtandaoni.

Namba hizo zitazuiliwa kupokea na kutoa huduma za mawasiliano isipokuwa kama watumiaji watazihakiki kwa kutumia vitambulisho vyao vya uraia kabla ya muda huo.

Novemba 2022, TCRA ilitangaza kuzifunga namba tambulishi 52,087, zikiwemo zile zinazohusishwa na wizi, utapeli na ulaghai kupitia mawasiliano ya simu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags