Lady Gaga alivyotinga vazi lililotengenezwa kwa nyama

Lady Gaga alivyotinga vazi lililotengenezwa kwa nyama

Ubunifu ni kati ya kitu muhimu kwa wasanii kama njia ya kuwapa utambulisho na kuwafanya waendelee kujitengenezea utofauti. Ili kuwa na utofauti wapo waliowekeza ubunifu kwenye mavazi au mionekano yao kwa ujumla.

Ikiwa leo ni Alhamisi siku ambayo baadhi ya watu hukumbuka matukio yaliyotokea siku za nyuma, kwenye upande wa burudani yapo matukio mengi ya kukumbukwa lakini kati ya hayo ni hili la mwanamuziki wa Marekani Lady Gaga kuvaa nguo iliyotengenezwa kwa kutumia nyama mbichi ya ng'ombe.

Ili kujipa utofauti, Lady Gaga alivaa vazi hilo kwenye Tuzo za MTV Video Music zilizofanyika Septemba 12, 2010 na kusababisha kuzua mijadala kuhusiana na matumizi hayo ya nyama kama sehemu ya vazi.

Vazi hilo lililobuniwa na Franc Fernandez na kutengenezwa na Nicola Formichetti, makundi ya watetezi wa haki za wanyama walionesha kuchukizwa nalo, lakini liliorodheshwa na Time kama vazi lililofanyiwa ubunifu wa juu zaidi kwa mwaka 2010.

Kama ilivyo kawaida ya mavazi yake mengine, vazi hilo lilihifadhiwa sehemu maalum, na lilikuja kuoneshwa tena mwaka 2011 kwenye Rock and Roll Hall of Fame baada ya kuhifadhiwa na wataalamu wa taxidermy kama aina ya nyama iliyokaushwa.

Baadaye, vazi hilo lilipelekwa kwenye Newseum Washington D.C. Mwaka 2019, vazi hilo lilioneshwa Las Vegas katika makumbusho ya Haus of Gaga ndani ya kasino ya Park MGM.

Lady Gaga alizaliwa mwaka 1986 na kuanza muziki rasmi mwaka 2001, tayari amefanya ngoma kama vile Bloody Mary, Bad Romance, Judas na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags