Kylie Jenner ajutia kufanya Surgery

Kylie Jenner ajutia kufanya Surgery

Mrembo na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani @kyliejenner amekiri kuwa alifanya upasuaji wa matiti alipokuwa na umri wa miaka 20 na anajutia kufanya hivyo wala hatamani binti yake aje kufanya kama alivyofanya yeye.

Baada ya kukanusha kwa muda mrefu kila alipokuwa akiulizwa kuhusiana na yeye kufanya upasuaji wa matiti hatimaye akiwa katika kipindi cha “The Kardashian” mrembo huyo alikiri kwa kumwambia rafiki yake kuwa alifanya upasuaji wa matiti akiwa na umri wa miaka 20 kabla ya kumpata binti yake Stormi,

Katika maongezi yake Kylie alisema,

“Najutia sana kufanya hivyo natamani ningebaki na matiti yangu ya asili,na kama kuna mtu anafikiria kufanya hivyo napendekeza asubiri mpaka apate watoto

Nina mtoto wa kike pia na mrembo sana nitaumia sana moyo kama akitaka kufanya kama nilichokifanya katika umri mdogo , natamani kuwa mama mzuri kwake na niwe mfano kwake”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags