Kimaumbile inaelezwa kwamba, mwanaume hahusishi tendo la kujamiiana na kumpenda mwanamke.
Kwa mwanaume, kupenda ni jambo moja na tendo la kujamiiana ni jambo lingine. Hii ni tofauti na wanawake ambao wanaonekana kuunganisha tendo la kujamiiana na kupenda.
Ndiyo maana katika hali kama hiyo, unaweza kukuta mwanaume anatoka nje, anafumaniwa na mkewe, badala ya kuwa mjeuri huomba radhi sana nap engine hutoa zawadi kubwakbwa ili kumbembeleza mkewe asimwache.
Anaweza kufumaniwa hata mara tano, lakini bado akaendelea kuomba radhi na kunyenyekea sana kwa mkewe. Mtu anaweza kujiuliza, kama anamtaka au bado anampenda huyo mke wake, ni kwa nini ameamua kutoka nje, tena siyo mara moja?
Ni kwamba mwanaume hatembei na mwanamke kwa sababu anampenda, bali anaweza kuoa mwanamke kwa sababu anampenda. Kutembea na mwanamke, kwa mwanaume ni suala la haja ya mwili kujiridhisha na labda udadisi kutaka kujua umbo la mwanamke la aina hii lina ladha gani kimapenzi lakini siyo kupenda.
Unaweza kukuta wanaume wengine wanatembea na wanawake lukuki, lakini wakifika nyumbani wanakuwa na adabu zao.
Kwa wanawake hali siyo hiyo, na ndio maana mwanaume akimfumania mkewe, inabidi ajue kwamba, kupendwa kumeisha au kumefifia sana. Hii ni kwa sababu kwa mwanamke kupenda na tendo la ndoa ni kama kitu kimoja. Kwa mwanamke kama hampendi mwanaume, kufanya naye mapenzi ni vigumu, labda tu kama amempendea fedha na anazihitaji sana ili kumaliza matatizo yake ya kifedha au anafanya biashara.
Ndiyo maana wanaume wanapowafunia wanawake huumia zaidi na huweza kuchukua hata hatua mbaya, ukilinganisha na hatua wanazochukua wanawake.
Hata kama mwanamke aliyetoka nje ataomba radhi na kudai kwamba, alitoka kwa bahati mbaya na mazingira yanaonyesha hivyo, bado mwanaume atasukumwa na kitu asichokijua kuamini kwamba, sababu pekee ya mpenzi wake kutoka nje ni kujirahisisha.
Kwa kudhani kutoka nje ni kujirahisha na kukosa thamani, mwanaume humchukulia mke au mpenzi wake kwa thamani ya chini sana. Ndiyo maana huanza kumwita Malaya, kahaba na majina mengine yanayofanana na hayo.
Kwa mwanamke hali ni tofauti, yeye akifumania anataka kujua huyo mwanamke aliyemchukua mumewe au mpenzi wake anamzidi kitu gani.
Hii ni kwa sababu, akilini kwa mwanamke huamini kwamba kuna kitu kilichomvutia mumewe au mpenzi wake kwa huyo mwanamke aliyemfumania ambacho yeye hana.
Mwanamke atajitahidi kujilinganisha ili kutafuta kile kilichomvutia mumewe kwa mwanamke huyo, na ndipo hapo maswali kama haya hujitokeza. “Hivi ulimpendea nini yule mwanamke..? au “ Ni kitu gani ulichokikosa kwangu mpaka ukakifuata kwa yule mwanamke…..?”
Leave a Reply