Kwa nini mahusiano ya kimapenzi hayaepukiki kazini

Kwa nini mahusiano ya kimapenzi hayaepukiki kazini

Kazi kazi ndiyo kauli inayotamba mjini, na sisi Mwananchi Scoop tupo hapa kukujuza kadha wa kadha kuhusu maswala ya kazi na leo tupo hapa kwa ajili mambo ambayo hayaepukiki, kuhusiana na kwa nini mahusiano hayaepukiki kazini ungana nasi kupata dondoo kamili.
Mapenzi mapenzi mapenzi nimeyaita mara tatu hili jambo ni kama pembe la ng’ombe halifichiki, mtajitahidi kutunza siri lakini ni pembe hilo lazima lichomoze, waswahili wanasema penzi kikohozi hahahaha, nacheka kama matamu.

Jambo sugu linaloshawishi mahusiano ya kimapenzi katika eneo la kazi ni mazoea yailiopitiliza. Si vyema kumtumia mwenzako emoji ya kukonyeza kupitia ujumbe (sms).
Ukaribu huo ambao mara nyingine unachochea mapenzi ofisini haukuwezekana wakati wa janga la corona, wakati wengi walikuwa wanafanya kazi nyumbani.

Licha ya hayo, wafanyakazi wamepata njia ya kuendelea kutaniana na wenzao, jambo ambalo linaonyesha kutoepukika kwa mahusiano ya mapenzi ofisini au mahali pa kazi.

Februari 2022 data kutoka Jumuiya ya Marekani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (SHRM) inapendekeza mahusiano ya mapenzi ya mahali pa kazi yanaweza kuongezeka hata wakati wa kufanya kazi nyumbani.

Theluthi moja ya waliohojiwa kati ya 550 walijibu kwamba walianza uhusiano na wenzao wakati wa janga hilo, ongezeko la 6% kutoka siku kabla ya janga la kiafya duniani.

Mahali pa kazi ni msingi mzuri wa mapenzi na ni mapenzi ya muda mfupi, ilhali kampuni nyingi hazipendi mahusiano ya kimapenzi kazini.

Wataalamu wanasema kuna sababu maalum ambazo wafanyakazi hawawezi kuacha kushirikiana na wenzao, hata wakiwa wametengwa wakati wa janga la corona.



Ingawa mahusiano ya kazini hayaruhusiwi kabisa, 75% ya wale waliojibu uchunguzi wa SHRM walisema ni sawa kwa mtu kuwa na mahusiano.
Baada ya yote, nusu walisema walipenda mwenzao wakati fulani. Ingawa ni changamoto kubwa kwa kampuni nyingi, mapenzi kati ya wafanyakazi yamekuwepo kwa karne kadhaa.

Lakini wanandoa wengi hukutana kazini mfano mzuri Obama na mkewe walikutana katika ofisi ya sheria ya Chicago walipokuwa na umri wa miaka 20.

Takwimu za mwaka 2017 zinaonesha kuwa mmoja kati ya wenzi 10 wenye mahusiano ya mapenzi nchini Marekani wanasema walikutana kazini.

Kwa kuzingatia kwamba baadhi ya data zinaonesha kwamba kati ya watu wenye umri wa miaka 20 na 50 hutumia karibu mara nne ya muda mwingi na wafanyakazi wenzao kuliko marafiki, hii inaonekana kuwa lazima kutokea.

“Haishangazi kwamba watu wengi wanakuwa wapenzi kazini, kwa kuwa kazi imekuwa ikichukua muda wetu zaidi na zaidi kwa miaka mingi” anasema Vanessa Bohns, profesa wa tabia ya shirika katika Chuo Kikuu cha New York, kutoka Cornell, Marekani.

Urafiki na kufahamiana
Mahali pa kazi kunachochea mvuto wa mahusiano, anasema Amie Gordon, profesa wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Michigan ambaye anasoma saikolojia ya mahusiano.
Kutumia wakati mwingi na mtu kuna uwezekano mkubwa wa kufungua njia ya mahusiano ya mapenzi, kwa sababu ya mambo yote ambayo tunajua yanachangia urafiki na kufahamiana.

Kwanza, kadiri tunavyoona kitu (au mtu), ndivyo tunavyozidi kukipenda au kumpenda. Sifa hii ya kufahamiana ni upendeleo wa kisaikolojia, kuonana na mtu mara kwa mara kunaweza kusababisha mvuto, anasema Gordon.

Vile vile, utafiti umeonesha kuwa karibu na mtu kwa muda mrefu kunaweza kusaidia kuchochea upendo kwa mtu, kadiri tunavyomwona mtu kimaumbile na jinsi mwingiliano zaidi tunaona, ndivyo mvuto wa watu wengine unavyoongezeka haraka.

Upendeleo huo unaweza kutumika hata kwa waajiri wanaopendelea wafanyakazi ambao hutumia wakati mwingi nao. Pia ni ukaribu wa kihisia na ukaribu wa kiakili, iwe ni kupitia barua pepe au Zoom, bado wanakuwa karibu.

Hali hiyo ya kila mara na mwingiliano huchochea upendeleo, bila kujali eneo halisi, ambapo unaweza kueleza kwa nini mapenzi ya ofisini yamedumu katika kipindi cha kufanya kazi kwa mbali.

Sababu nyingine ambayo inapita ofisi ni upendeleo wa watu kwa wale wanaofanana nao, ambapo inaweza kuongeza kazi, kwa kuzingatia kwamba wenzake walichagua kazi sawa na kampuni.

Matokeo ya mapenzi kazini
Ingawa mapenzi ya ofisini hayaepukiki na yanakubaliwa na watu wengi, bado ni ngumu. Kwanza kabisa, inaweza kuongeza hatari ya unyanyasaji wa kijinsia, mazingira ya uadui kazini, pamoja na kuunda migogoro ya kimaslahi. Mara nyingi zaidi, mapenzi ya ofisini yanaweza pia kufanya timu nyingine kukosa raha na kuathiri utendakazi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags