Kupiga picha wahanga wa ajali faini milioni 100

Kupiga picha wahanga wa ajali faini milioni 100

Nchini Dubai ukipiga picha watu waliojeruhiwa au miili ya watu waliofariki katika ajali ni kosa linaloweza kusababisha kifungo cha miezi sita jela na faini ya tsh 100 milioni, au vyote kwa pamoja.

Pia, yeyote anayetumia simu ya mkononi, kompyuta au njia za mtandaoni kurekebisha au kuhariri video au picha ya mtu mwingine kwa lengo la kumchafua anaweza kufungwa mwaka au faini kati ya tsh. 170 milioni.

Hiyo inalenga kuimarisha ulinzi wa jamii dhidi ya uhalifu unaofanywa kupitia matumizi ya mitandao na majukwaa ya Teknolojia ya Habari nchini humo.

Kwa hapa Tanzania sheria ya Kanuni za adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022 chini ya Kifungu cha 162(1) (a) (b) kinakataza kuchukua, kusambaza picha, video, au taswira za miili watu waliofariki, waathiriwa wa uhalifu au matukio ya kutisha ila kwa madhumuni maalum kama uchunguzi wa jinai.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags