Kundi la Hakuna Matata lafuata nyayo za Ramadhani Brothers

Kundi la Hakuna Matata lafuata nyayo za Ramadhani Brothers

Kundi la waruka sarakasi kutoka Tanzania liitwalo ‘Hakuna Matata Acrobats’ wanaendelea kufuata nyayo za ‘Ramadhan Brothers’, hii ni baada ya kutua kwa kishindo katika hatua inayofuata kwa kupewa Golden Buzzer kutoka kwa jaji Sofia Vergara.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram wame-share video wakati wa mashindano hayo huku ikiambatana na ujumbe ukieleza kuwa kupita kwao kwa kishindo hicho huenda ikiwa nafasi nzuri ya kulikalibia taji la America’s Got Talent (AGT) msimu wa 19.

‘Hakuna Matata Acrobats’ ilitangaza nia yao ya kushiriki katika mashindano hayo ya kusaka vipaji April mwaka huu ikiwa ni wiki chache tuu kupita tangu kundi la ‘Ramdhani Brothers’ kushinda taji la AGT Fantasy.

‘Hakuna Matata’ wanaungana na ‘Ramadhani Brothers’ kuwa Watanzania pekee ambao wamefanikiwa kushiriki katika mashindano hayo ambayo hukusanyisha watu kutoka kwenye mataifa mbalimbali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags