Kundi la Daz Nundaz kukiwasha Bongoflava Honors julai 22

Kundi la Daz Nundaz kukiwasha Bongoflava Honors julai 22

Ikiwa ni mwendelezo wa tamasha la muziki la ‘BongoFlava Honors’, linalosimamiwa na mwanamuziki mkongwe Joseph Mbilinyi 'Sugu', awamu hii ni zamu wa wanamuziki wa zamani kutoka kundi la ‘Daz Nundaz’ ambao watatumbuiza Julai 19 2024.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Sugu amechapisha video akilitambulisha kundi hilo ambalo lilikuwa la watu wanne akiwemo Daz Baba, Ferooz, K!SAL na Sista P ambapo baadhi ya wasanii katika kundi hilo wanatarajia kutumbuiza kwa mara ya kwanza toka wafanye show miaka 22 iliyopita.

Utakumbuka kuwa tamasha la Bongoflava Honors mara ya mwisho lilifanyika Aprili 26, 2024 katika ukumbi wa Warehouse Arena.tz Masaki likiwakutanisha mastaa kama AY, Mwana FA na Weusi katika jukwaa moja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags