KUMBUKIZI: Siku ya wakimbizi duniani

KUMBUKIZI: Siku ya wakimbizi duniani

Machafuko, vita na mateso vinafanya zaidi ya watu milioni 80 duniani kote kufungasha virago na kuzikimbia kaya zao huku wakiacha kila kitu kwa ajili ya kuokoa maisha yao na ya familia zao, katika kuepukana na adha ya vurugu na machafuko. 

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), idadi ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao imeongezeka kila mwaka katika miaka 10 iliyopita.



Aidha siku ya wakimbizi duniani huadhimishwa kila Juni 20, kusherehekea ujasiri wa watu ambao wamelazimika kukimbia nchi zao na makazi yao. Kwa mwaka 2022, maadhimisho yamejikita katika haki ya kutafuta usalama.

Wakati wowote watu wanapolazimika kukimbia makazi yao, wana haki ya kulindwa dhidi ya vita, vurugu au mateso kwani kila mtu anastahili kuwa hai na salama.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags