Kula kadri ya mahitaji, usipitilize

Kula kadri ya mahitaji, usipitilize

Kijana mwenzangu unatambua kuwa kuna njia rahisi ya kupunguza tumbo haraka na inaweza isikufanye ukae na njaa kwa siku nzima.

Kabla hatujaendelea ni muhimu kukumbuka aina hii ya kupunguza tumbo au unene unayoenda kuisoma haitakiwi uiache baada ya muda mchache.

Ili upate mafanikio ya kudumu unashauriwa kuifuatilia kwa muda mrefu zaidi.

  1. PUNGUZA KULA SUKARI NA VYAKULA VYA WANGA KWA UJUMLA.

Kutokula sukari kwa wingi na vyakula vya wanga kunasaidia kupunguza njaa hivyo kunafanya upunguze kiasi cha chakula unachokula.

Kwa sababu miili yetu hutumia wanga kutengeneza nguvu ya kujikimu na shughuli zote za mwili, uhaba wa fungu hili la chakula mwilini husababisha miili yetu kutafuta mbadala wa kutengenezea hii nguvu kwa ajili ya uhai.

Kwa hiyo miili yetu huamua kutumia glycogen na mafuta ambayo yanakuwa yametunzwa mwilini ambayo yanafanya tuonekane wanene ili kutengeneza nguvu kwa ajili yetu.

Mafuta yanapotumika kutengeneza nguvu badala ya wanga ndipo tutaona mabadiliko ya kupungua mwili.

 

 

 

Pia kupunguza vyakula vya wanga kunaleta kupungua kwa hormone ya insulin. Hii inasababisha figo kuondoa chumvi na maji mwilini hivyo kama tumbo limejaa linapungua haraka sana.

Kwa kifupi kupunguza vyakula vya wanga automatically vinaulazimu mwili uyeyushe mafuta!.

  1. KULA PROTINI, MBOGA MBOGA NA MAFUTA YA MIMEA.

Ulaji wa protini, mbogamboga na mafuta ya mimea kunachangia au kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tumbo.

Hakikisha kila mlo wako una protein, kuanzia chakula cha asubuhi.

Chai na chapati/maadazi/vitumbua/cutlets/mihogo/viazi/keki/ kipi sijataja hapo? achana navyo kabisa. Kila mlo lazima uwe na protein na mbogamboga.

Mfano wa vyakula vyenye protini: Nyama ya ng’ombe, kuku, mbuzi, Samaki: Salmon, sato, sangara, prawns, Mayai: Ya kuku wa kienyeji ni mazuri zaidi

Vyakula vya aina ya protein vinafaida kubwa sana katika kupunguza uzito wa mwili.

Utajisikia kushiba kwa muda mrefu, hamu ya kula kula hovyo au kula usiku wa manane vitapungua sana hivyo kukufanya kula kwa kiasi.

Kwa upande wa mboga mboga vyenye wanga kidogo ni kama, Cabbage, broccoli, Spinach, Mchicha, Cauliflower, lettuce.

 

Usijinyime mboga mboga katika kila mlo kwasababu zina nyuzinyuzi ambazo zinasaidia pia kukufanya ushibe haraka, pia zina vitamins na madini mengine muhimu zinazohitajika mwilini.

  1. FANYA MAZOEZI MARA KWA MARA

Ukipunguza vyakula vya wanga na mengine mengi niliyokwambia hapo juu ni muhimu kuhakikisha unafanya mazoezi pia.

Siyo lazima ufanye mazoezi kila siku ila iwe mara kwa mara pia ukifanya mazoezi sanasana ya weight lifting matokeo yatakuwa makubwa zaidi.

Unaweza kufanya mazoezi ya cardio kama jogging, kuendesha baiskeli, kuogelea. Angalizo unaweza kuchagua siku moja tu katika wiki kula vyakula vya wanga kama wali/ugali/viazi/chapati n.k

Ukifanya hivyo utaongezeka uzito kidogo tu ambao unasababishwa na maji kwasababu kula vyakula vya wanga kunafanya mwili ushilikile maji mengi, ukipunguza tena vyakula hivi figo itatoa hayo maji na uo uzito kidogo ulioongezeka utatoka.

Kwa hiyo jitahidi ujicontrol usipitilize siku moja tu ya kula hivi vyakula vya wanga, na pia usifanye maajabu kwa kula hadi kupitiliza kama kulipizia. Ni muhimu kujifunza kujicontrol.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags