Kofia ya MJ kupigwa mnada kwa zaidi ya 34 milioni

Kofia ya MJ kupigwa mnada kwa zaidi ya 34 milioni

Kofia ya aliyekuwa mwanamuziki wa Pop nchini Marekani Michael Jackson aliyoivaa kwa mara ya kwanza wakati akitumbuiza ‘dansi’ yake ya Moonwalk imepigwa mnada na sasa iko sokoni nchini Paris kwa ‘dola’ 82,000.

Kwa mujibu wa NDTV news inaeleza kuwa kofia hiyo nyeusi aina ya Fedora imekadiriwa kuuzwa kwa Euro 60,000 hadi 100,000 na mnada wa Hotel Drouot.

Kofia hiyo ikiwa ni kivutio kikubwa kati ya vitu 200 vya msanii huyo vya kumbukumbu ingawa kitu chake kilichouzwa kwa bei ya juu zaidi ni gitaa lake ambalo linamilikiwa na Bluesman T-Bone Walker.

Inasemekana kuwa mkali huyo wa Pop alivua kofia hiyo wakati akicheza wimbo wa Billie Jean katika tamasha la Motown mwaka 1983 wakati akicheza ‘staili’ yake ya kurudi kinyumenyume ya Moonwalk.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags