Kocha wa soka la vijana ashambiliwa na mzazi

Kocha wa soka la vijana ashambiliwa na mzazi

‘Kocha’ wa ‘soka’ la vijana wa Virginia, Vince Villanueva adaiwa kupigwa na mzazi aliyetoka nje ya uwanja na kumvamia kwa kumpiga na chupa ya maji usoni na kusababisha majeraha makubwa, ikiwa ni pamoja kupasuliwa sehemu ya jicho.

Inasemekana tukio hilo la kushtua lilitokea baada ya kutokea  mzozo wa ‘timu’ hiyo ya wavulana baada ya ‘Kocha’ Vince  akijaribu kufanya mabadiliko kwenye mchezo.

Baada ya kufanya mabadiliko hayo ya wachezaji katika mchezo huo ndipo mzazi wa moja ya wachezaji alitoka na kwenda kumchukua mwanaye na kumrudisha mchezoni huku ‘Kocha’ akibaki anashangaa kitendo cha mzazi huyo.

Hata hivyo mzazi huyo  alimtaka ‘kocha’ pembeni  kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo hapo ndipo mazungumzo yalibadilika na kuwa ngumi.

Mzazi huyo aitwaye Bletand Hoxha mwenye umri wa miaka 45, yupo mikononi kwa polisi kwa shambulio hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags