Kocha wa Mamelodi achukia kuingiliwa majukumu yake

Kocha wa Mamelodi achukia kuingiliwa majukumu yake

Kocha wa Mamelodi Sundowns F.C., Rulani Mokwena achukizwa kuingiliwa kwenye majukumu yake baada ya mkurugenzi wa klabu hiyo #FlemmingBerg kuwaondoa wachezaji wanne ambao bado walikuwa katika mipango yake.

Tovuti ya Sky Sport News imeeleza kuwa Mokwena hajafurahishwa na #Mamelod kumpa mamlaka mkurugenzi kuwatema wachezaji hao ambao bado alikuwa na mipango nao kueleeka msimu ujao.

Wachezaji hao waliotolewa katika ‘klabu’ hiyo ni Brian Onyango, Zungu, Gaston Sirino pamoja na mshambuliaji Thabiso.

‘Kocha’ huyo pia hajafurahishwa na kitengo cha ‘timu’ hiyo kumpa thamani Mkurugenzi wa michezo katika usajili na yeye kutopewa kipaumbele.

“Kuna mchezaji nilimtaka lakini ‘bodi’ wamegoma kumsajili hivyo wanaingilia majukumu yangu na wamewaondoa wachezaji ambao binafsi bado ninamipango nao” Rulan

Hata hivyo ‘kocha’ huyo mwenye umri wa miaka 37 tayari amewaambia kama hawatompa uhuru wa kuitengeneza ‘timu’ basi atajiweka kando na ‘timu’ hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags