Usiku wa kuamkia leo, umezuka moto katika Kituo cha Mafuta cha Ovis Kigamboni Darajani Dar es Salaam huku chanzo cha awali kikidaiwa kuwa ni ufaulishaji holela wa mafuta.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatmah Nyangasa amewatoa hofu Wakazi wa Kigamboni kwamba hadi sasa hali ni shwari kwani moto huo umeunguza malori mawili ya mafuta na sio matenki ama Kituo cha Mafuta kama taarifa zilivyosambazwa awali.
"Niwatoe wasiwasi Wananchi wetu Wakazi wa Kigamboni, hali ni shwari na kilichotokea ni ajali ya moto iliyohusisha magari mawili na sio Kituo cha Mafuta ama matenki ya mafuta kama ambavyo taarifa zilikuwa zikisambaa lakini cha kumshukuru Mungu hakuna madhara makubwa kwa Binadamu” amesema Fatma Nyangasa
Aidha aliendelea kwa kuelezea kuhusiana na walinzi walioko eneo la tukio na kusema kuwa “Vijana wetu wawili ambao ni Walinzi wa eneo hili wamepata mshtuko ambapo Wataalamu wa Afya wanawahudumia hapa, hakuna Mtu aliyepoteza maisha tunamshukuru Mungu kwa hilo” amesema Mh Fatma Nyangasa
Leave a Reply