Kiswahili chatumika kwenye wimbo wa Rema

Kiswahili chatumika kwenye wimbo wa Rema

Mwanamuziki kutoka Nigeria Rema ametumia Lugha ya Kiswahili kwenye wimbo wake mpya uitwao ‘Heis’ ikiwa kama zawadi kwa mashaabiki zake na wadau wanaopenda muziki wake kutoka Afrika Mashariki.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mwanamuziki huyo ameshare kipende cha wimbo huo pamoja na jina la wimbo huku akiwa ameweka imoji za bendera tatu ikiwemo Tanzania, Kenya na Rwanda, akimaanisha wimbo huo uwafikie mashabiki zake kutoka Afrika Mashariki.

Baada ya ku-share wimbo huo baadhi ya mashabiki walijitokea kupitia uapende wa ‘komenti’ wakifurahishwa na kitendo hicho ambacho kiliongeza mvuto kwenye kionjo cha wimbo wake huo ambao bado haujawekwa kwenye platifom yoyote.



Hii siyo mara ya kwanza wa wasanii kutoka mataifa mbalimbali kutumia lugha ya Kiswahili katika nyimbo zao utakumbuka mwazoni mwa mwezi Mei mwaka huu ‘Rapa’ Gunna kutoka Marekani aliachia wimbo uitwao ‘Hakuna Matata’ akiwa ametumia maneno hayo kama jina la wimbo wake.

Inafahamika kuwa "Hakuna Matata" limetokana na lugha ya Kiswahili, likiwa na maana ya kuwa "hakuna shida" au "hakuna wasiwasi".

Katika wimbo huo wa Rema ametumia maneno ya Kiswahili kama ‘Ni wewe’, ‘Ni nani anabamba, ni nani mkali sana’ ‘Ni nani ndio bingwa na mengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags