Kutokana vazi la abaya kutrendi kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakidai kuwa ni lazima kuvaa vazi hilo katika sikukuu ya Eid El Fitr, Mkurugenzi wa Taasisi ya Al-Hikma Shekh Nurdeen Kishk ameweka wazi kuwa uvaaji wa vazi hilo siyo lazima katika siku hiyo.
Kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari Kishk ameeleza kuwa siyo lazima uvae abaya mpya katika sikukuu ya Eid El Fitr kuna namna nyingi ya kusherehekea siku hiyo mfano kuketi na mumeo mkiwa na furaha na siyo kukasirikiana kisa umekosa Abaya.
Abaya ni vazi linalovaliwa juu ya nguo kama pazia la mwili, ni vazi la wanawake hususani wa Kiarabu, waswahili huliita vazi hilo baibui.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply