Kinda Mtanzania ana kwa ana na Arshavin

Kinda Mtanzania ana kwa ana na Arshavin

Kinda wa Tanzania, Harrith Chunga Misonge aliyepo Russia anakoshiriki mashindano ya Games of the Future amekutana na staa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Russia, Andre Arshavin ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mechi za mashindano hayo jijini Kazan.

Arshavin alionekana kuvutiwa kimaongezi na Harrith ambaye ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Aghakhan ya jijini Dar es salaam na kuzungumza naye kwa dakika zisizopungua kumi

"Aliniuliza nafasi ninayocheza lakini pia aliniuliza nchi ninayotoka akaniambia kwamba amewahi kufika Zanzibar na alivutiwa na fukwe zake alizozifananisha na fukwe za Maldives" alisema Harrith.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 12 amewekwa katika timu ya Franklins Bumblebee ambayo inajumuisha wachezaji watano kutoka katika mataifa mbalimbali duniani huku akionyesha kiwango cha kuvutia
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags