Kimbunga Fredy chauwa 14, Msumbiji na Madagascar

Kimbunga Fredy chauwa 14, Msumbiji na Madagascar

Takribani watu 7 nchini Madagascar na 7 Msumbiji wamepoteza maisha baada ya kimbunga Freddy kupiga.

Kulingana na ripoti ya hivi punde ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), idadi ya watu walioathiriwa na Kimbunga Freddy imeongezeka hadi 383, 000 kwa jumla huku (226,000 nchini Madagascar na zaidi ya 163,300 nchini Msumbiji).

“Japokuwa nguvu ya Kimbunga Freddy haikuwa kama tulivyotarajia, mamia na maelfu ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu . Ahueni itachukua miezi kadhaa” Pasqualina Di Sirio, Mwakilishi wa WFP na Mkurugenzi wa Nchi wa Madagascar alieleza hilo.

Kuna uwezekano wa mafuriko kusini mashariki mwa Zimbabwe kwani kimbunga Freddy hakikuweza kuenea kama ilivyotabiriwa hapo awali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags