Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kimbunga cha kitropiki kukumba pwani ya mashariki ya Madagascar, huku mvua kubwa ikiambatana na upepo mkali kuangusha mapaa ya nyumba na kusababisha dhoruba kali.
Ofisi ya Kitaifa ya kudhibiti majanga ilisema mwanaume mwenye umri wa miaka 27 alizama kwenye bandari ya Mahanoro, Mashariki mwa Madagascar.
Kimbunga Freddy kimetua Jumanne, wiki kadhaa baada ya dhoruba lingine la kitropiki kuua watu 33 na kuwaacha maelfu bila makazi baada ya kupasua nyumba na uwanja wa michezo wa Maranjary.
Maelfu ya watu wamehamishwa kutoka Mkoa wa Vatovavy, wa kwanza kupigwa na zoruba hili. Mvua kubwa, upepo mkali sana, bahari iliyochafuka na mafuriko ya pwani yanatarajiwa kuendelea katika maeneo ya hatari.
Vimbunga vya kitropiki hupoteza nguvu zao vinaposogea nchi kavu. Utabiri wa hali ya hewa unatabiri kuwa kimbunga Freddy atadhoofika kwa dhoruba kali ya kitropiki kitapoelekea Msumbiji, Jumatano.
Hata hivyo, nchi ya kisiwa cha Bahari ya Hindi iko katika hatari kubwa ya vimbunga. Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini ilionya kuwa mvua kubwa itaendelea kunyesha.
Leave a Reply