Kilichotokea kwa Kane siyo hat-trick

Kilichotokea kwa Kane siyo hat-trick

Hat-trick ya kwanza iliyodaiwa kufungwa na Star wa ‘klabu’ ya #BayernMunich #HarryKane yakataliwa kutokana na sheria za ‘soka’ nchini Ujerumani zinazotaka ili iwe hat-trick ni lazima mchezaji afunge bao tatu mfululizo.

Mchezaji huyo aliisaidia ‘timu’ yake kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya ‘klabu’ ya Vfl Bochum kwenye Uwanja wa Allianz Arena huku ikidhaniwa kuwa alifunga hat-trick.

Kumbe haikuwa hivyo Kane alifunga bao lake la kwanza katika dakika ya 12 kisha akaongeza mabao mawili kipindi cha pili. Hata hivyo, hat-trick hiyo haikuhesabiwa kwa sababu tayari kuna mchezaji alifunga bao katikati ya mabao mawili aliyofunga Kane.

Hivyo basi kutokana na hayo haijakubalika kwani ili iwe hat-trick Kane alitakiwa kufunga mabao matatu mfululizo bila ya mchezaji mwingine kufunga.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags